Mwimbaji wa muziki wa Injili ambaye pia ni mtangazaji nyota wa kituo cha redio cha Praiz Power cha jijini Dar, Victor Aaron (kulia) akiongea na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa albamu yake iitwayo Hujaanza Wewe unaotarajiwa kufanyika Oktoba 11 mwaka huu ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee. Albamu hiyo ina nyimbo 10 ambazo ni Mkatae ama Mkubali, Msilale, Tuwe na Huruma, Wokovu, Udongo bila Maji, Nani katika Mbingu, Nimesogea Pamoja na Ni kwa Neema.
Victor atasindikizwa na wasanii kibao wa Gospel nchini ambao ni pamoja na Bony Mwaitege, Bahati Buku, Christna Shusho, Janeth Benny, Jenifffer Mgendi na Ambwene Mwasongwe Kushoto ni Noel Leonard mratibu wa uzinduzi huo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: