Yule mchekeshaji maarufu Bongo na bingwa wa kuiga sauti za watu maarufu hapa Bongo na sehemu nyinginezo duniani Steve Mengere maarufu kwa jina la Stive Nyerere, anasema mwaka mpya wa 2009 ni mwaka wa mabadiliko kwake na anasema ni vyema kwa wasanii wenzake kuboresha kila kitu katika maisha kuanzia katika kazi za usanii, maisha, tabia na mavazi.Stive aliyasema hayo wakati akiongea na habari na matukio katika kukitambulisha kipindi chake kipya ambacho kitaanza kurushwa hivi karibuni katika Luninga kupitia kituo cha TBC.
"Nataka nifanye mambo kimataifa zaidi ndio maana nimeamua kuanzisha show yangu ambayo nina uhakika itakuwa babkubwa, wapenzi na washabiki wangu watulie tu mambo mazuri kibao yapo kwa ajili yenu." alisema Nyerere.Jina la Stive Nyerere limetokana na sanaa yake kwa kuwa alianza usanii kwa kuingiza sauti ya Baba wa Taifa ,Mwalimu Julius Nyerere.
Meneja wa Steve ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kurekodi movie na vipindi bwana Hartman Mbilinyi anasema kila kitu kiko tayari kilichobaki ni kuanza kuonekana kwa kipindi hicho.Zaidi ya Nyerere Steve pia ana uwezo wa kuwaigiza watu maarufu kama Bin Laden, Rais wa Marekani Bwana George Bush, na wengine wengi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: