Wanafunzi wa chuo kikuu sehemu ya Mlimani(UDSM) leo mchana wamekamatwana na kutiwa mbaroni baada ya kuandamana kinyume cha sheria wakiwa na mabango yakuushutumu uongozi wa chuo hicho.
Habari na matukio wakiwa kwenye eneo la tukio walishuhudia vurugu kubwa baina ya wanafunzi na askari wa kutuliza ghasia FFU kwenye eneo hilo.

Kwa ujumla hali ni tete katika eneo hilo mpaka Habari na matukio inaondoka ilishuhudia jumla ya wanafunzi watano wakikamatwa na kutiwa ndani ya gari la askari hao na kuondoka nao eneo hilo kwa kuwapeleka kituo cha polisi cha Mlimani.

Katika mabango hayo kama yalivyosomeka mengi yalikuwa yakiwalaumu viongozi wa chuo hicho kwa kushinikiza kuwarudisha Chuoni hapo bila masharti wanafunzi hao, ikiwa ni pamoja na kushinikiza Mkuu wa chuo hicho Prof Mukandala kujiuzulu.

Naye Rais wa DARUSO akiongea kwa niaba ya wenzake walisema wataendelea kubeba mabango mpaka wahakikishe watoto wa Maskini nao wanapata haki ya kuendelea na Masomo.Naye Mkuu wa Chuo hicho Prof Mukandala alisema uongozi wa chuo umeongeza siku badala ya mwisho wa masharti ambao ulikuwa leo badala yake umesogezwa mpaka tarehe 29 ya mwezi huu.

Wadau mnasemaje kuhusu sakata hili la wanafunzi hawa....??Nini kifanyike....??
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: