Rais wa Miss Tourism World, Wrganisation John Singh (kati) akipeana mikono na mh. Aloyscious Gonzaga Mandago huku Isaack Kassanga akionesha mkataba ambao kampuni ya Easy Finance ambayo wao ni wakurugenzi imeingia na hiyo taasisi inayoendesha mashindano ya urembo ya utalii duniani.Sherehe hii ilifanyika katika ofisi za Easy Finance iliyoko kinondoni, jijini Dar es Salaam.
kwa mujibu wa makubaliano hayo, Easy Finance, ambayo pia ni mmoja wa wafadhili wakuu wa globu ya jamii ya issamichuzi.blogspot.com, sasa itakuwa msimamizi wa mashindano ya Miss Tourism kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia Januari 2009.

Pia itasimamia na kuendesha, kupitia taasisi ingine ya nyumbani, mashindano ya Miss Tourism ya bongo. Hali kadhalika itaandaa fainali za dunia za mashindano hapa bongo mwakani ambapo zaidi ya nchi 70 zitashiriki.
Hivyo taasisi iliyokuwa ikiongozwa na Gideon Chipungahelo kwa miaka sita iliyopita haitohusika tena na uandaaji wa Miss Tourism hapa nyumbani. Habari zinasema kuwa taasisi mpya itakayochukua nafasi ya ile ya Chipungahelo imeshaanzishwa na Easy Finance na mambo yakienda mswano Tiss Tanzania 1994 wa pili Lucy Ngongoseke kihwele ndiye atakayekuwa anaiongoza.

Toa Maoni Yako:
0 comments: