MKUU wa mkoa wa Manyara BW. HENRY SHEKIFU ametoa wito kwa vyama vyote vya siasa vitakavyoshiriki katika uchaguzi mkuu ujao mkoani MANYARA viweke wawakilishi wao katika vituo vyote vya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kujiridhisha na zoezi hilo.

Bw. SHEKIFU amesema hatua hiyo ni muhimu kwasababu itasaidia kupata picha halisi ya zoezi zima la uandikishaji na uboreshaji wa daftari hilo hivyo kuondoa malalamiko yasiyo ya msingi wakati wa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Amesema wajibu wa wawakilishi wa vyama hivyo vya siasa ni kuangalia kama sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi zinazingatiwa katika uandikishaji na akawaonya wawakilishi hao kutowaingilia watendaji wanapotekeleza wajibu wao.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Manyara kujitokeza kwa wingi kujiandikisha wakati wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Septemba 22 mwaka huu katika kanda ya Kaskazini.

Bw. SHEKIFU alikuwa akizungumza mjini Babati na maafisa waandikishaji na maafisa waandikishaji wasaidizi wasaidizi wa mkoa wa Manyara, wakati akifungua semina iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: