
Rais Jakaya Kikwete yupo Mkoani Manyara kwa ziara ya Kikazi ya Siku sita,ambapo amekagua Miradi mbalimbali katika sekta ya kilimo,afya,maji na barabarana kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi kadhaa ya kiuchumi na kijamii Mkoani humo na kuzungumza na wananchi wa wilaya zote za Simanjiro, Kiteto, Babati, Hanang na Wilaya ya Mbulu kabla ya kuhitimisha ziara yake na kurejea jijini Dar es Salaam September 17----------------
RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ametoa wito kwa watanzania kutumia huduma za kibenki kuweka akiba na kujipatia mitaji kwaajili kukuza shughuli zao za kiuchumi na kibiashara ili kuharakisha maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla.
Amesema watanzania wasiogope kukopa kwenye asasi za fedha kwasababu njia ya kukopa ili kuongeza mitaji ya kibiashara imekuwa ikitumiwa na wafanyabiashara duniani kote na maendeleo yao yanaonekana kukua kwa kasi.
Rais Kikwete amesema hayo mjini Babati wakati akiweka jiwe la msingi na kuzindua tawi la Benki la NBC Babati katika ziara yake ya kikazi ya siku 6 mkoani Manyara, ambapo pia alikabidhi mikopo yenye thamani ya shilingi Bilioni 3 na milioni 30 kwa Halmashauri ya mji wa Babati na asasi ya walimu ya Manyara Group Limited.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Christo De Vries amesema benki yake itaendelea kiwango cha utoaji mikopo na kusaidia shughuli za kijamii ambapo kila mwaka, benki hiyo imepanga kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 kusaidia kazi za maendeleo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: