Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila (pichani), jana alishambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara. Mchungaji Mtikila alishambuliwa mjini Tarime alipokuwa akiwanadi wagombea wa chama chake wa Udiwani na Ubunge.

Habari zilizopatikana kutoka huko jana jioni zilisema kua, Mchungaji Mtikila alipatwa na mkasa huo wakati akizungumzia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (CHADEMA), marehemu Chacha Wangwe kwamba kilisababishwa na watu fulani.

Kwa mujibu wa habari hizo, Mchungaji Mtikila alipata maeraha kadhaa kichwani ambapo alipelekwa katika zahanati ya Tarime na kushonwa nyuzi tatu na Dk. Philemon Hugilo.

Aidha, ilielezwa kwamba, Mchungaji Mtikila alilazimika kuvalishwa shuka nyeupe kutokana na nguo zake alizokuwa amevaa, kutapakaa damu. Habari zaidi zilisema watu wanne wametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: