Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana, Ijumaa, Julai 18, 2008 alipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.

Ujumbe huo umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Kilimo wa Kenya, William Ruto wakati walipokutana kwenye makao makuu ya Jimbo la Mkinga, mkoani Tanga, katika eneo la Kasera.
Katika mkutano huo nyumbani kwa mkuu wa wilaya hiyo, Ruto amewasilisha kwa Rais Kikwete salamu na ujumbe maalum kutoka kwa Rais Kibaki. Waziri Ruto amefuatana na Balozi wa Kenya katika Tanzania, Boaz Mbaya.

Waziri Ruto pia amemshukuru Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), kwa mchango mkubwa katika usuluhishi wa mgogoro mkubwa wa siasa uliolipuka kufuatia tofauti kubwa zilizotokana na uchaguzi mkuu nchini humo Desemba mwaka jana.
Ruto alimfuata Rais Kikwete mkoani Tanga ambako Rais Kikwete anaendelea na ziara ya mkoa huo. Ruto ameondoka Tanga kurejea nyumbani Kenya baada ya kuwa amewasilisha ujumbe huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: