Kwa mara nyingine tena tunakutana kupitia safu hii maridhawa kabisa ambayo tunazungumzia mada mbalimbali zinazogusa maisha yetu ya kimapenzi.

Nina imani kwamba umzima na mambo yako yanakunyookea huku ukiyafurahia maisha yako ya kimapenzi na yule umpendaye.

Kikubwa ambacho nimekuwa nikisisitiza hasa katika dunia hii ya sasa, ni watu kujitahidi kuwa na mapenzi ya kweli dhidi ya wapenzi wao na kuondokana na tamaa zisizokuwa na msingi.

Nasema hivyo kwasababu, magonjwa ni mengi sana kiasi kwamba kama hutatulia na mpenzi wako mmoja na kuangalia ni jinsi gani mnaweza kuishi maisha yenu kwa furaha, kubaliana na mimi tu kwamba, maisha yako yatakuwa ni mafupi.Ukimwi uko kila pembe, warembo na mabrazameni unaowaona huko mtaani wote wameathirika ambaye yuko salama ni wewe tu na mpenzi wako. Kwa maana hiyo, tulia na mpenzi wako na ridhika na kile unachokipata kutoka kwake.

Mpenzi msomaji wangu, kuna katabia ambako nimekabaini nimeona nitakuwa sijafanya busara kama nitaamua kukanyamazia. Ni hii tabia ya baadhi ya watu wanapobaini kuwa wapenzi wao wana vijisenti, hubweteka na kujigeuza tegemezi kwao. Hii ipo kwa jinsia zote si wanaume wala wanawake.

Si ajabu leo hii ukamsikia mwanamke akilalamika kuwa, jamaa yake amekuwa akimpiga mzinga kila siku tena wengine wanatumia nguvu. Wapo wanaume ambao wanalishwa, wanavalishwa, wamepangishiwa vyumba na wapenzi wao na hata kupewa fedha za matumizi. Hao wapo hasa sehemu za mijini.

Lakini leo nataka kuwazungumzia wanawake ambao wamegeuka kuwa kero kwa wapenzi wao kutokana na tabia ya kila wakati kuomba wasaidiwe na wapenzi wao bila kujali kwamba hali ya kifedha inaruhusu ama laa.

Sote tunajua kwamba, asilimia kubwa ya wanawake wanawategemea wapenzi wao katika mambo fulani yanayohitaji pesa. Achilia mbali wale ambao wana kazi licha ya kwamba nao kuna wakati wanaomba wasaidiwe. Lakini sana kuna wengine wanaboa bwana katika hili tuseme tu ukweli. Unaweza kusikia msichana akimtumia sms hii mpenzi wake:

“Dear naomba leo ukija uniletee choculate baadaye si utanipeleka steers? Nimekumiss sana” Kabla hujajibu anakuunganishia “samahani nilitaka kusahau naomba unitumie vocha nataka kuwasiliana na mama” Unamaliza kuitikia kwa unyonge anahitimisha “uwahi mpenzi tutoke”

Msichana wa namna hii ndiye ninayetaka kumzungumzia leo katika safu hii. Wapo baadhi ya wanaume hukacha kuonana na wapenzi wao kwa kudanganya kuwa wamesafiri, wako bize na kazi, kumbe hakuna lolote, wanakwepa kupigwa mzinga

Mambo hayo yapo sana, karibu wanaume wengi wanakabiliana nayo, wawe wameoa au wale ambao wana wapenzi tu. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna baadhi ya wanaume wanapoteza mahaba kwa wake zao kwa sababu ya kubanwa katika suala zima la matumizi. Wengine huamua kutoa talaka au kusitisha uhusiano, si kwa sababu hawapendi bali wamezidiwa na utegemezi wa wale wanaowapenda.Labda nikupe tu mbinu kadhaa zinazoweza kukusaidia wewe mwanaume ambaye mpenzi wako amezidi kukuchuna.

Wakati mwingine mwambie SINAWapo wanaume ambao hawajui kukataa kila wanachoombwa wanatoa, eti wanaona aibu kusema SINA! Akiombwa vocha analeta, kuku, kila kitu, hata kama hana fedha atakopa!

Lakini pamoja na ukarimu huo mazingira yanayojengeka kwa mwanamke ni ya tofauti ambayo yatakufanya siku huna kitu unyimwe penzi au wewe mwenyewe ujifanye umesafiri. Hili halitakiwi hata kama unazo wakati mwingine mwambie huna!

Kuwa muwaziInashangaza baadhi ya wanaume huongopea wenzao kwa kuwaambia wana mali hii na ile wakati ni waongo. Ni makosa kufanya hivyo sema ukweli...Itaendelea wiki ijayo, Kwa maoni 0713070116

Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

Naye akusaidie wakati mwingineJambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wake zao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mkewe ana kazi yake. Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.

Usifuje pesaKuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo. Unachotakiwa mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji.

Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie. Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kere. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo upukana na tabia hiyo.

Niishie hapo kwa leo, tuonane tena wiki ijao kwa mada nyingine lakini kwa ushauri zaidi unaweza kunicheki kwenye namba 0713070116 au email:zekaima@yahoo.com
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: