Pichani na Ma-Mc wakiendesha hafla hiyo ya utoaji tuzo katika kilele cha utoaji wa tuzo kwa wanamuziki wa zanzibar zilojulikana kwa jina la TIGO Zanzibar music Awards zilizofanyika kwenye ukumbi wa Salama bwawani hoteli, ambapo mgeni rasmi alikuwa mama Salma Kikwete.
Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation ambaye pia Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Mohammed Seif Khatib akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni yake.
Meneja wa Zanzibar Entertainment ambao ndio waandaji wa tuzo hizo, Bi. Saida Ally Seif baada ya kupokea tuzo kwa niaba ya kampuni.
Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation ambaye pia Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Mohammed Seif Khatib, akimkabidhi zawadi ya heshima mgeni rasmi wa tuzo hizo Mama Salma Kikwete.
Katibu mtendaji wa baraza la sanaa Zanzibar Mohamed Baramia (kati)akiwa pamoja na kundi la Akhanato Family baada ya kuibuka na tuzo ya kikundi bora cha kizazi kipya 2008.
Mama Salma Kikwete akimkabidhi tuzo ya mwanamuziki wa taarab asilia Mohamed Mohamed Machapara kuwa msanii wa bora wa mwaka 2008 ya TIGO music Awards iliofanyika katika ukumbi wa Salama hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Mbarak Abdalah Mgeni a.k.a Black Berry akiwa na tuzo yake albamu bora ya mwaka aliojinyakulia.Mwanamuziki Jamila Ally a.k.a Baby J akiwa amekamatia tuzo zake mbili kama unavyoona pichani mara baada ya kuzinyakua katika tuzo za Tigo Zanzibar Music Awards 2008.
Msanii chipukizi wa kizazi kipya aitwaye Haji Juma Haji a.k.a Manyota akiwa na tuzo yake ya mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka 2008.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: