Rais JK akiwa pamoja na makamanda wa Polisi. Wa pili kutoka kushoto ni IGP Mwema. Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa tume lililoiunda kuchunguza vurugu zilizotokea katika uchaguzi mdogo waUbunge katika jimbo la Kiteto imemaliza kazi yake najarada linatarajiwa kupelekwa kwa mkurugenzi wamashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya ushauri zaidi.Msemaji wa jeshi hilo Bwana ESAKA MGASA amesema leojijini Dar Es Salaam kuwa jarada la uchunguzi huolinaandaliwa kwenda kwa DPP wiki ijayo.
“Tume kwa ajili ya kuchunguza vurugu zilizotokeakatika uchaguzi Kiteto imemaliza kazi yake. Nitaratibu wa kawaida kwa IGP kutafuta ushauri wa DPP kabla ya kutoa uamuzi wowote,” amesema.
Vurugu hizo zilihusisha wafuasi wa CCM na CHADEMAwakati wa kampeini za uchaguzi mdogo uliofanyikaFebruari 24, 2008 kufuatia kifo cha mbunge aw zamani wajimbo hilo Benedict Lusurutia.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi nchinilimewatahadhalisha wananchi kuwa makini katika kipindihiki cha sikukuu kwa kuweka ulinzi wa kutoasha katikanyumba zao.
Msemaji wa jeshi hilo amewaambia waandishi wa habarijijini Dar Es Salaam leo kuwa hata ikiwezekana baadhiya watu waachwe kulinda nyumba zao wanapokwenda katikaibada za mauled na Mkesha wa Pasaka ili kuzuiawahalifu kutumia mwanya huo kutimiza malengo yao.
Msemaji wa Jeshi hilo Bwana Mgasa amewataadharisha piamadereva wa magari na watumiaji wengine wa barabarakuwa makini na kutolewa na kuheshimu sheria za usalamabarabarani ili kuepuka vifo visivyo vya lazima.
Amesema, “ madereva wa teksi wanatakiwa kuwawaangalifu sana kwa abiria wanaokodi magari hayo nakutokubali kwenda njia za uchochoroni hasa nyakati zausiku kwasababu wakati kama huu hutumiwa na waharifukuiba magari na kuhatarisha maisha ya madereva teksi.
”Kwa mujibu wa Msemaji huyo, wamiliki wa mabaa nagrocery nao wanatakiw akuzingatia taratibu na sheriakuhusiana na masharti yaliyoainishwa katika leseni zaoza biashara na kusitisha huduma mara moja muda wakufunga utakapofika ili kuepuka matukio ya kuvamiwa nakuporwa mali zao au za wateja wao.
Aidha jeshi hilo limewahaidi wananchi kuwalitaimarisha ulinzi nchi nzima na hasa katika sehemuzote za ibada nyakati za usiku.
Jeshi hilo limewataka wananchi wote wenye mapenzi memakutoogopa kutoa taarifa za watu wanaowatilia mashakaya kuwa wanataka kutenda uhalifu katika maeneo yao.


Toa Maoni Yako:
0 comments: