Wanajeshi wa Tanzania bada ya kufika Comoro kuongeza nguvu. Wanajeshi wa Jeshi la Wananchi Wa Tanzania wameendelea kuwasili katika visiwa vya Comoro kuungana na wenzao waliokwishatangulia kuendesha operesheni maalumu ya kumtoa muasi wa kisiwa cha Anjuani Kanali Mohamed Bakari.
Wakitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mjini Moroni wa Price Said Ibrahim kwa ndege ya JWTZ, wanajeshi hao wameonekana kuwa na mori kubwa ya kuungana na wenzao kutoka nchi za Sudan na Senegal ili kupambana na Kanali Bakari.
Mara baada ya kuwasili kwa wanajeshi wa Tanzania muda mfupi tu iliwasili ndege ya serikali ya Libya iliyowabeba askari wa Sudan na baadae kusafirishwa kwa amagari maalumu ya jeshi kuelekea katika makambi ya muda katika kisiwa cha Comoro.
Magari ya jeshi ya Comoro na Tanzania yalitumika kuwasafirisha wanajeshi hao hadi katika makambi yao ya muda katika mji wa Moroni.
Askari kutoka Senegal wanatarajiwa kuwasili katika visiwa vya Comoro muda wowote ili kukamilisha idadi ya askari 1800 walioahidiwa na Umoja wa Afrika kuisaidia serikali halali ya Jamuhuri ya Visiwa vya Comoro.
Hadi hivi sasa majeshi ya Umoja wa Afrika yaoongozwa na majeshi ya Tanzania hayajatoa taarifa maalumu ni lini watakivamia kisiwa cha Anjuani kumuondoa Mohamedi Bakari aliyejitangazia uraisi.

Habari kwa Hisani ya Stanley Ganzel aliyeko huko Comoro.

Toa Maoni Yako:
0 comments: