Wakitengeneza chakula chaoPichani ni chakula aina ya chochoni lakini kwa wale wasukuma wanaita Michembe wanachotumia wakazi wa Micheweni, Zanzibar Kaskazini. Baada ya kukumbwa na njaa.
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itapeleka chakula cha kutosha kwa wananchi wa Shehia nne za Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika jitihada za kukabiliana na upungufu wa chakula unaowakabili baadhi ya wananchi wa Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi, Afisi ya Waziri Kiongozi mhe. Machano Othman Said amesema chakula hicho kitapelekwa haraka iwezekanavyo kuwaweza wananchi kuondokana na tatizo la ukosefu wa chakula, uliosababishwa na ukame wa muda mrefu.
Mhe. Machano ametoa kauli hiyo baaada ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na upungufu wa chakula ikiwa pamoja na shehia za Micheweni, Majenzi, Mjini Wingwi na shehia ya Shumba Mjini.
Aidha amesema licha ya msaada huo wa chakula serikali tayari imeshapeleka wataalamu kufanya utafiti ili kupata ufunguzi wa kudumu kuhusu tatizo la upungufu wa chakula, linalowakumba wananchi wa Wilaya hiyo kila mwaka kutoakana na maumbile ya ardhi ya eneo hilo na ukame.

Toa Maoni Yako:
0 comments: