Mkurugenzi wa Kundi la TOT na Mbunge wa Mbinga Mashariki, Kapteni (mstaafu) John Komba, amekiri kumtosa mkewe Mwalimu Salome Komba na kukimbia majukumu ya kifamilia.
Kapteni Komba alitoboa siri hiyo ya kumtosa mkewe hivi karibuni, wakati wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Bakili Muluzi, iliyopo Boko Dar es Salaam walipoitembelea shule hiyo. Shule hiyo inamilikiwa na Komba.Shuhuda wetu aliyekuwepo katika ziara hiyo alisema, wakati wakiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara hiyo, Komba aliinuka na kuomba kuzungumza mbele ya hadhara na kukubaliwa.
Chanzo chetu hicho kilimkariri Komba akianza kutoa risala jinsi wanaume wengi wanavyosababisha maumivu kwa wake zao, hasa kutokana na kusahau majukumu ya kifamilia.
“Njoo mke wangu nikuombe msamaha mbele ya wazazi wenzangu, maana nilikosa ndio maana leo najuta na ninajutia dhambi zangu nilizozitenda bila kujua.
“Wazazi wenzangu hawa watoto ndio mboni zetu, tusiwaache waishi maisha kama ya ndege ya kula chini na juu, jukumu letu ni kuhakikisha wanapata elimu bora.
“Mimi ilifika kipindi nilijisahau kuhusu majukumu yangu katika familia, lakini mke wangu alifanya kazi ya ziada na kuhakikisha hatupati fedheha ili watoto wasome,” alisema Komba huku akimkumbatia mkewe na kububujikwa na machozi.
Komba aliomba muongoza sherehe ampigie kibao cha ‘Siku hazigandi’ wa Lady Jaydee, ambacho ndicho kilichomliza zaidi.“Kukimbia kwa Komba katika majukumu ya kifamilia ina maana ni kumtosa mkewe na kuacha kila kitu akifanya mwenyewe, ni heri yeye amekiri kuliko wengine wasiotaka kufanya hivyo,” alisema mzazi mmoja aliyeomba kutotajwa jina.
Aliposakwa baadaye ili afafanue zaidi kuhusu kukimbia majukumu ya familia, Komba aliomba kuachwa kwa kile alichodai aachwe kwa kipindi hicho.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: