
Trekta ambalo linafanya kazi ya kukarabari barabara ya Simu 2000

Barabara inayofanyiwa maerekebisho.
Na Mathias Canal, Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo leo (Machi 19, 2017) amezuru na kufanya ukaguzi wa barabara ambayo ipo kwenye matengenezo ya dharura.
Barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya wananchi waendao Sinza, Mpaka Mwenge na Posta hadi Kariakoo sawia na Tegeta hadi Bagamoyo Pwani na Wengine kuelekea Ubungo hadi Morogoro ijulikanayo kama simu 2000 iliyopo katika Kata ya Sinza Manispaa ya Ubungo imeanza kutengamaa kwa gari kupita pasipo wasiwasi zaidi ya ilivyokuwa awali.


Toa Maoni Yako:
0 comments: