Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wakwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: