Katapila likibomoa moja ya nyumba nne zinazomilikiwa na Mchungaji Getrude Rwakatare katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam jana.
WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Makazi jana imebomoa nyumba nne zilizojengwa ndani ya kiwanja namba 314 zilichopo eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam zinazomilikiwa na Mchungaji Getrude Rwakatare kwa tuhuma kuwa alivamia eneo hilo. Kazi hiyo ya ubomoaji, ilitekelezwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi na iliendeshwa kwa pamoja na maofisa wa Ardhi kutoka wizarani na Manispaa ya Kinondoni, waliodai wamepewa agizo hilo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Alphayo Kidata.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: