1Mwimbaji wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga wakati wa Tamasha la Pasaka lililofanyika mkoani humo likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili, Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Msama Promotion na linaendelea Kesho kwenye uwanja wa CCM Kirumba ambapo Mwanamuziki maarufu wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Rebecca Malope atafanya mambo mamkubwa jijini Mwanza. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-SHINYANGA) 2Kundi la wanenguaji wa mwimbaji Rose Muhando wakifanya vitu vyao kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo. 3Mwimbaji Rose Muhando akicheza na watoto wakati alipokuwa akiimba katika Tamasha la Pasaka mjini Shinyanga leo. 4Mwimbaji wa muziki wa injili Upendo Kilahiro akiimba jukwaani huku akipigwa tafu na waimbaji wenzake wa muziki wa injili kutoka kushoto ni Grace Mwikwabe, Tumaini Njole, Faraja Ntaboba kuoka nchini Congo DRC na Mess Chengula. 5Mwimbaji Upendo Nkone wa pili kutoka kulia akicheza na waimbaji Faraja Ntaboba kulia na wenzake Grace Mwikwabe kushoto na Tumaini njole wakati alipokuwa akifanya vitu vyake jukwaani 6Faraja Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 7Faraja Ntaboba mwimbaji wa muziki wa injili kutoka Congo DRC akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 8Mwimbaji Mess Chengula naye alifanya mambo makubwa katika tamasha hilo. 9Mess Chengula akionyesha uwezo wa ktawala jukwaa katika tamasha hilo. 10Mwimbaji Grace Mwikwabe akifanya vitu vyake ambapo kesho anatarajiwa kuzindua albam yake kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 11Mwimbaji Tumaini Njole amefanya mambo makubwa pia. 12Mashabiki wa muziki wa injili waliohudhuria katika tamasha hilo wakipata burudani kutoka kwa waimbaji mbalimbali katika tamasha hilo. 13Hapa ni Full burudani
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: