Vitabu vya Dini vinamuita MKE ni MSAIDIZI WA MWANAUME

MSAIDIZI kwa Kiingereza ni HELPER - Mtu anayekupa Msaada na kukutoa kwenye Stage moja kwenda Nyingine iliyo bora zaidi, Anayekufanya Uwe bora zaidi kuliko Mwanzo, anayekufanya Uongezeke Zaidi. Swali ni Je, Wewe ambaye unategemea Mwanaume Fulani Akuoe ili ukawe MKE, Una tabia za KISAIDIZI (HELPING BEHAVIOUR)??? Au ndo walewale KANTANGAZE TYPE??

Tangu uwe nae kama Rafiki na sasa Mchumba, UMEMSAIDIA NINI?? Umemkuta hana hata nusu heka ukamsaidia Ku-Invest for Future Use yenu au umekuwa Mtaalamu wa Ku-Suggest Kiwanja gani kipya muende kula Bata??

Umemkuta anakaa chumba kimoja cha Kupanga, Umemsaidiaje upande wa SAVING ili ahamie in a better house au Awe na Nyumba yake mwenyewe ambayo in Future itakuwa YENU???

Badala ya kumsaidia KUSAVE wewe ndio umekuwa BIBI TOBOA TOBO, umetoboa Mfuko wake wa Mshahara kwa Bili zako za Saluni, Peruvian Hair, Kodi yako ya Nyumba, Viatu na Handbags kutoka China na kuvijaza chumbani kwako kama uko Show Room, Matokeo yake miaka na miaka Kabwana hakana SAVING na kana Mikopo kwenye kila Benki, SACCOSS na VICOBA... AND YOU CALL YOURSELF A WIFE MATERIAL... Tena unalalamika kabisa, jamaa mwaka wa 7 huu hata hasemi lolote... ANAKULIA TIMING TU.

You are a BIA Material.... Mke sio Mihips, Sura na kope bandia, NI TABIA YA KISAIDIZI iliyo ndani yako ndio inahesabu.

WARNING:
Unaweza ukamsaidia na Asikuoe, akaoa mwingineeee... Usilalamike, Kila mtu ameandikiwa mtu wake, wewe umetumika kama Tuition tu, Mtihani akafaulu mwingine! Sio kila aliyefaulu NECTA ana akili, wengine waliiba Mitihani!

Imetolewa na
Mkuu wa Chuo cha Mapenzi.
Seth De Jesus Giovanni, Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: