Gari la Dar Express lenye namba za Usajili T 580 CFP leo Mei 9, 2014 limepata ajali mida ya saa nne eneo la Wami likitokea Dar es Salaam kwenda nchini Nairobi, Kenya. 

Kwa mujibu wa Mashuhuda wa ajali wakitoa taarifa za awali walisema kuwa gari hilo lilipinduka baada ya basi hilo kuyumba na kujikuta likipinduka japo hawakujua kilichofanya mpaka hayo yote yakatokea.

Katika ajali hiyo hakuna aliyekufa zaidi ya abiria kadhaa kupata majeruhi kutokana na kuchomwa na vioo vilivyopasuka. Habari kamili zitawajia punde tutakapokamilisha taarifa kamili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: