Kaimu mwenyekiti wa Uukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda akizungumza na wanandishi wa habari leo Agosti 27, 2014 juu ya mwenendo wa bunge la katiba.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Wakati mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo, nao Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) wazidi kumtupia lawama zote za kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mheshimiwa Samweli Sitta na kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama kikao cha Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania Hebron Mwakagenda amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifuatilia mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.

Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano Bw Mwakadenga amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa
watanzania,
 “Kwanza bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini uchunguzi wetu unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika na kusaini kwenye kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100 tuligundua kuwa hawapo bungeni wakiwemo mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya viongozi wa kamati”amesema Mwakagenda.

Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya bunge hilo kuvurugika ni pamoja na kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa, matumizi mabaya fedha ikiwa ni pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni, kukosekana kwa theluthi mbili toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye rasimu mambo ambayo amesema kuwa mwenyekiti Samweli Sitta ameyafumbia macho na kijifanya kama hayaoni huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.

“Huyu mzee hatujamwelewa kabisa, sisi tumekaa tumezungumza naye tukamuuliza atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe watapatikana wapi hajatupa jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambaye
ameshachanganyikiwa, anapambana na kila anayekuja mbele yake, iwe mwandishi, mwanaharakati, mbunge, yeye amekaa kujihami tu, sasa hali hii sio nzuri kwa mchakato muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi Kikwete kiusimamisha mchakato huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na kuonekana wazi kuwa hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi ambayo sisi kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba bora, “Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa, uchaguzi wa serikali za mitaa, daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa, hii haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa katiba hautawezekana tena, sisi tunamwomba mheshimiwa Rais Kikwete awasikilize watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.

Mchakato wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma bila ya mariano na wajumbe waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais amekubali kukutana nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya akiweka jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani –Mziha sehemu ya Magole-Turiani (48.6km) inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe, mbunge wa Mvomero Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya kina kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kabla ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Magole-Turiani (48.6km) kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Profesa Juma Kapuya wakifurahia jamabo na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mheshimiwa Antony Mbasa kabla ya uzinduzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto wakifurahia kikundi cha ngoma za asili mara baada ya Mheshimiwa Rais kuwasili Wilaya ya Mvomero kwa ajili ya kuzindua ujenzi wa Barabara ya Magole-Turiani (48.6km).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wa kwanza (kushoto) akizungumza kabla ya uzinduzi rasmi wa barabara ya Magole Turiani. Wa kwanza kulia kwake ni Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Ndyamukama pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi na Umeme Dkt. Wiliam Nshama.

Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, Chuo cha Diplomasia kimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano ‘PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS’ kati ya tarehe 18 – 22 August, 2014. 

Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya muda mfupi yatolewayo na Chuo cha Diplomasia kila mwezi, katika mafunzo hayo ambayo kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika Chuo cha Diplomasia, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao.

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoa na Balozi Sanga (mwenye Kaunda suti katikati)

Mafunzo hayo yalihusisha maofisa wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali, Chuo cha Ardhi, Jeshi la Wananchi, Magereza, Ubalozi wa Uingereza, na sekta binafsi kama Benki Kuu ya Tanzania, SMART TANZANIA (Telecom), SERENA HOTEL, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Chuo cha Utalii Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Umoja wa Mataifa (UN),

Mafunzo hayo ya juma moja yaliyofanyika Kurasini Dar es salaam, washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma.

Akifunga mafunzo hayo, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bw. Juma M. Kanuwa alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao.

“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa umma (Protocol and Public Relations) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na Chuo cha Diplomasia yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,” alisema.

Akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji mafunzo haya yatarudiwa tena Zanzibar mnamo mwezi wa kumi, yakifuatiwa na ‘INTERNATIONAL SECURITY AND ARMS CONTROL, FRENCH LANGUAGE na DATA COLLECTION AND ANALYSIS (Using SPSS, SQL and STATA) hapa chuo cha Diplomasia, na kuwataka wale wote wanaohitaji wafike chuoni ama kupiga namba 0713667303 au cfrshortcourse@yahoo.com kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.
Washiriki wa mafunzo kutoka Chuo cha Ardhi na Chuo cha Utalii Tanzania wakipokea vyeti vyao.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
---
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumpiga risasi mwendesha piki piki aliyejulikana kwa jina la Salgo Ndunguru(22) mkazi wa Ruvuma mjini Songea.

 Akizungumza kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amesema tukio hilo limetokea Agosti 26 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea ambapo askari polisi wawili PC Waziri mwenye namba G 5075 na PC Ayoub mwenye namba G 9800 wakiwa doria na piki piki ya polisi yenye namba za usajili PT 1250 CR aina ya Yamaha CC 250 katika eneo hilo la Kombezi walimjeruhi mwendesha piki piki huyo kwa kumpiga risasi.

 Amesema mwendesha piki piki huyo alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari PC Waziri katika harakati za kuinsuru silaha hiyo iliyokuwa imebebwa na askari mwenzake PC Ayoub ambaye alizingirwa na baadhi ya waendesha piki piki wakiongozwa na mwendesha piki piki aliyejulikana kwa jina moja la Agrey ambaye alidai kuwa yeye ndiye mmiliki wa piki piki iliyokamatwa na askari hao ikiwa imebeba mzigo wa majiko.


 Ameitaja piki piki iliyokuwa ikiendeshwa na majeruhi huyo kuwa ni aina ya San Lug yenye namba za usajili T 757 CUD ambapo baada ya mwendesha piki piki huyo kukamtwa alimpigia simu mdhamini wake Agrey alipofika alisababisha mkusanyiko mkubwa wa waendesha piki piki maarufu kama Yebo yebo ambao walianza kuwarushia mawe askari hao huku majeruhi akiwa ameshika mtutu wa bunduki iliyokuwa imebebwa na askari PC Ayoub ndipo askari PC Waziri katika kuinusuru silaha isiporwe alimpiga risasi majeruhi kwenye kiganja cha mkono wa kushoto na risasi hiyo kumjeruhi sehemu mbili ambazo ni kiganja cha mkono wa kushoto na paja la mguu wa kushoto.


 Amesema majeruhi amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri na katika vurugu hizo zilizodumu kwa muda wa nusu saa kabla ya kutulizwa na kikundi cha askari maalumu kilichowahi na kutuliza vurugu hizo kwa kutumia nguvu kidogo hali ikarejea kuwa shwari na hakuna madhara zaidi yaliyojitokeza.

Aidha kamanda Msikhela amesema uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo unaendelea na hatua zitachukuliwa dhidi ya wahusika watakaothibitika na ametoa wito kwa waendesha piki piki kuacha tabia ya kushabikia vurugu ambazo hazina tija na kuwa chanzo cha kusababisha migogoro isiyokuwa na maana na kusababisha madhara kwa jamii.

 Amewataka waendesha piki piki kufuata taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi husika kwa kupitia viongozi wao ili yaweze kufanyiwa kazi amewataka wananchi mkoani Ruvuma kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote kwani jeshi la polisi liko imara kulinda mali na maisha yao.

Mhe. Meya Wills akipokelewa na Bw.Suleiman Saleh, Afisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano waTanzania, Washington DC mara baada ya kuwasili Ubalozini hapo kwa mazungumzo na Mhe. Balozi Liberata Mulamula

Mhe. Liberata Mulamula,Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika mazungumzo na Mhe.Arnell Wills, Meya
wa mji wa Helena-West Helena, Arkansas, Marekani,Ubalozini Tanzania House, Washington DC.
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Meya Wills zawadi maalum kutoka Ubalozini.
.Mhe. Mulamula akiwa katika picha ya kumbukumbu na Mstahiki Meya Wills wa Mji wa Helena –West Helena, Arkansas, Marekani. 

Balozi wa Jamhuri ya Muungano nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula jana Jumanne Agosti 26, 2014, alikutana na Mhe. Mstahiki Meya wa Mji wa Helena-West Helena kutoka jimbo la Arkansas, Marekani, Ubalozini “Tanzania House” Washington DC. Mhe. Wills ambaye  Mji wake wake wa  Helena-West Helena una mahusiano ya kidada (Sister City) na Mji wa Moshi, Tanzania, alifika Ubalozini ili kufahamiana na Mhe.Balozi Mulamula pamoja na kumuelezea mashirikiano yaliyopo baina ya Mji wa Helena-West Helena na Moshi ambapo makubaliano rasmi yalisainiwa Oktoba 12, 2012, hapa Marekani kufuatia ziara ya Mhe. Japhary Michael, Meya wa Mji wa Moshi katika mji wa Helena –West Helena, Arkansas.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Wills alimuelezea Mhe. Balozi Mulamula juhudi zake katika kuimarisha mashirikiano hayo ya miji hiyo miwili ambapo yamejikita zaidi katika sekta ya utalii pamoja na shughuli nyingine za kukuza uchumi. Balozi Mulamula alimshukuru Meya Wills kwa kumtembelea na kufurahishwa na Meya huyo kutokana na kutembelea Tanzania mara mbili na kupata ufahamu zaidi wa Tanzania na hivyo kusaidia kupanua mahusiano yaliyopo baina ya Moshi na Helena –West Helena. Mhe. Mulamula alimshauri Mhe. Meya Wills kupanua wigo wa ushirikiano huo katika sekta nyingine za uchumi, biashara na uwekezaji.
10349153_841207622565532_7288991937464718532_n

Unaweza kuwa humfahamu kwa vile hana kelele nyingi.... TUONYESHE UZALENDO KWA KUMPIGIA KURA SASA

Msanii bora wa muziki wa Reggae Tanzania, DABO (Pichani) amepata nafasi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa, baada ya kuchaguliwa kuwania tuzo kubwa kabisa za reggae za kimataifa na muziki wa dunia 2014 (International Reggae and World Music Awards (IRAWMA).

DABO anawania tuzo hizi katika kipengele cha Mtumbuizaji Mpya Bora, akikabiliwa na ushindani kutoka kwa wasanii MC Norman kutoka Uganda, Alkaline na Kranium kutoka Jamaica na Shatta Wale kutoka Ghana.
196441_588093307897900_104541301_n

Zoezi la kuwapigia kura wasanii hawa kuwawezesha kushinda linaendelea sasa mtandaoni. Link ya kumpigia kura ni: http://www.irawma.com/irawma_vote2014
DABO ametajwa kuwania kipengele cha Best New Entertainer
Kwenye kipengele hicho, DABO anachuana na
* Daniel Bambatta Marley - Jamaica
* MC Norman - Uganda, Africa
* Alkaline - Jamaica
* Kranium - Jamaica
* Shatta Wale – Ghana
Asante kwa Kuunga mkono zoezi zima ndio kama linaanza!
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiongoza kikao cha kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 4 ya Vijimambo ambayo imebeba ujumbe wa kutangaza maliasili na  utalii wa Tanzania na kukemea Ujangili wa wanyama pori na misitu sherehe inayofanywa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani pamoja na Jumuiya ya Watanzania DMV mgeni Rasmi atakuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa pamoja nae Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe. Saidi Ali Mbarouk. 
 Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bwn. Baraka Daudi, Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Afisa Suleiman Saleh na Katibu wa Kamati ya maandalizi Bi. Asha Nyang'anyi wakiendelea na mkutano uliofanyika kwenye ofisi katika jengo la Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Washington, DC siku ya Jumanne Aug 26, 2014.
 Afisa Ubalozi Suleiman Saleh na Bi Asha Nyang'anyi wakifuatilia mkutano.
 Bwn. Baraka Daudi na Mhe. Balozi Liberata Mulamula wakifuahia jambo. Picha kwa hisani ya Vijimambo

Meneja Takwimu Mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika leo Mkoani Iringa kuhusu zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda limeloanza rasmi leo wilayani Ludewa kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO - LUDEWA)

Na Veronica Kazimoto, Ludewa.

Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda waliopo katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi wakaopita katika viwanda vyao ili kufanya zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Iringa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Meneja Takwimu mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi amesema zoezi hilo linaanza rasmi leo tarehe 25 Agosti, 2014 na litamalizika siku ya Jumapili tarehe 31 Agosti, 2014.

“Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda wilaya ya Ludewa linaanza rasmi leo na litahusisha jumla ya kata kumi na sita ambazo ni pamoja na Ludende, Lugarawa, Ruhuhu, Lupanga, Lwela, Mavanga na Mundindi”, amesema Fundi.

Amezitaja kata nyingine kuwa ni, Ibumi, Mlangali, Kilondo, Madope, Lupingu, madilu, Makonde, Mkongobaki na Lifuma.
Fundi amefafanua kuwa taarifa zinazokusanywa katika zoezi hili kutoka viwandani ni pamoja na jina la kiwanda, anuani za kiwanda, mahali kiwanda kilipo, aina ya umiliki na utaifa wa mmiliki.

Taarifa nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi na gharama za uzalishaji.

Zoezi hili la Uorodheshaji wa Viwanda lilianza tarehe 8 Aprili, 2014 kwa Tanzania Bara na mpaka sasa karibu maeneo yote zoezi hili limekwisha kamilika.
 
Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado. Picha zote na www.sufianimafoto.com
 Wafanyakazi wanaume wa Kampuni ya Toyota Tanzania, wakishindana kukuna Nazi wakati wa Bonanza maalumu la kuwapongeza wafanyakazi lililoandaliwa na Kampuni hiyo lililofanyika kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, juzi Agosti 23, 2014. Katika Bonanza hilo timu ya Rav 4 iliibuka mshindi wa jumla katika michezo yote iliyochezwa ikifuatiwa na timu ya Hilux, VX na Prado.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la ushindi wa jumla katika michezo yote mwakilishi wa timu ya RAV 4, Mumma Nyamhanga, wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la washindi wa pili katika michezo yote mwakilishi wa timu ya Hilux,  Brian Manase, wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la washindi wa tatu katika michezo yote wawakilishi wa timu ya VX, Athuman Mgeni (wa pili kushoto) na Ibrahim Zombo (wa pili kulia), wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Toyota Tanzania,  Bw. Vinod Rustagi, akimkabidhi Kombe la washindi wa Nne katika michezo yote mwakilishi wa timu ya Prado, Mtumwa Amour (wa pili kulia) na Fazal Ismail (wa pili kushoto), wakati wa hafla ya Bonanza maalum la kuwapongeza wafanyakazi wa Kampuni hiyo lililofanyika kwenye ufukwe wa Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es salaam, mwishini mwa wiki. Kushoto ni mwamuzi wa michezo hiyo, Othman Kazi. 
 Timu ya Rav 4, ambao waliibuka na kikombe cha ushindi wa jumla, wakipiga picha ya kumbukumbu pamoja kwa furaha, baada ya kukabidhiwa kombe lao la ushindi wa Bonanza hilo lililoelezwa kuwa litakuwa likifanyika kila mwaka ili kuwapa motisha wafanyakazi wake.
 Timu ya PRADO....
 Timu ya VX....
 Timu ya HILUX......
 Timu ya RAV 4...........
 Wachezaji wa timu ya Rav 4 (wenye Tisheti za rangi ya njano) wakichuana kuwania mpira na wachezaji wa timu ya VX. Katika mchezo huo Rav 4 walishinda mabao 2-0.
 Chenga moja Chaliiiiiii..........................
 ''Hapa si ubosi tu hata soka bado nimo''.......
 Mtanange ukiendelea.....
 Wachezaji wa timu ya Prado (wenye Tisheti za rangi ya bluu) wakichuana kuwania mpira na wachezaji wa timu ya Hilux. Katika mchezo huo Prado walishinda kwa mkwaju wa penati baada ya kumalizika dakika 30 na kutoka sare ya bao 1-1.
 Mourinho wa timu ya Prado (kushoto) akifanya vitu vyake na kumgalagaza beki wa Hilux.
 Netiboli hapa ilikuwa ni timu ya Rav 4 (rangi ya njano) na Prado, Rav 4 ilishinda mabao 9-2.
 Hapa ilikuwa ni timu za Netiboli kati ya Hilux (rangi nyekundu) na VX, Vx ilishinda mabao 7-3
 Voliboli hapa ilikuwa ni Rav 4 na Prado...Prado walishinda.....
 Wahi hiyo weweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 Hapa ilikuwa ni mchezo wa kuvuta kamba kati ya VX na Rav 4, Rav 4 walishinda
 Timu ya Rav 4....
 Mvutano ulikuwa si wakitoto.......
 Hapa ilikuwa ni mchezo wa kudansi.....na kuganda......
 Kamba timu ya Prado.......
 Kamba timu ya Prado na Hilux......
 Soka, kipa wa timu ya VX, Maganga, akidaivu kudaka mpira mbele ya adui yake.