AFISA Kumbukumbu za Wanachama wa Mfuko wa PSSSF Bw. Alex Bwanakunu (kulia) akimsikiliza mwananchi aliyetembelea Banda la PSSSF kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza Agosi 2,2026

Dodoma, Agosti 2, 2026

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki katika Maonesho ya Nanenane 2026 kwa kutoa huduma mbalimbali na elimu kuhusu Hifadhi ya Jamii kwa wanachama wake na wananchi kupitia mabanda yake yaliyopo katika kanda tano nchini, ikiwemo Zanzibar.
Msanii maarufu nchini ,Mrisho Mpoto (wa pili kushoto) akiwa ameshika mkanda ,moja ya bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha KLICL,Kinachomilikiwa na PSSSF kwa ushirikiano na Jeshi la Magereza ,alipotembelea Banda la Mfuko wa PSSSF kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma Agosti 2,2026,kushoto ni Afisa Mkuu wa Uhusiano wa Mfuko wa PSSSF Bw.Abdul Njaidi na kulia ni Afisa Mauzo kiwanda cha KLICL, Bi. Mary Muna

Kwa mujibu wa Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, PSSSF imeshiriki maonesho hayo katika Kanda ya Kati viwanja vya Nanenane mkoani Dodoma, ambako Maonesho ya Nanenane 2026 yanafanyika kitaifa na tayari yamezinduliwa na Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Agosti 1, 2026. Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Tambua Soko; Ongeza Tija na Thamani ya Kuelekea Dira 2025’.
Wanachama wa Mfuko wa PSSSF wakihudumiwa kwenye Banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa kwenye viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma Agosti2, 2026.

Katika maonesho ya mwaka huu, PSSSF inashiriki; Zanzibar katika viwanja vya Dole, Kanda ya Magharibi mkoani Tabora katika viwanja vya Ipuli Mnadani, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza katika viwanja vya Nyamhungolo, Kanda ya Kusini mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya, viwanja vya Nanenane.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa PSSSF Bi.Esther Mpemba (kulia ) akimuunganisha Mwanachama wa PSSSF ,Bi.Maliasa Sajoho na Mfumo wa PSSSF Member Portal ambao unamuwezesha kupata huduma za mfuko Kidijitali,kwenye maonesho ya Nanenane Viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma Agosti 2,2026

"Tunawakaribisha wanachama wetu na wananchi wote kutembelea mabanda ya PSSSF katika kanda hizo ili kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu mafao, kuhakiki taarifa zao na michango, pamoja na kuwaunganisha katika huduma zetu za kidijitali, huku tukiwahakikisha kesho ya uhakika wanachama wetu’" alisema Bw. Njaidi.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa PSSSF ,Bi .Saluna Ally (kushoto) akimuhudumia Mstaafu anayepokea Pensheni PSSSF ,Bw.Mwakibete G.Kasilati,kwenye banda la mfuko huu katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye viwanja vya Nanenane Jijini Mbeya,Agosti 2,2026

Aidha, watakaotembelea kwenye mabanda ya PSSSF watapata nafasi ya kuona fursa za uwekezaji wa Mfuko ambazo ni pamoja na bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Kiwanda cha KLICL na nyama kutoka machinjio ya Kimataifa ya Nguru.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Mwigulu Nchemba akitoa hotuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa katika viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma Agosti 1, 2026.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Magharibi Bw.Eliadi Mndeme akitoa elimu kwa mwanachama wa PSSSF wakati wa Maonesho ya Nanenane Kanda ya Magharibi ambayo yanafanyika viwanja vya Ipuli mkoani Tabora Agosti 2, 2026.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: