Na Mwandishi Wetu.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Leo XIV, amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kufikisha umri wa miaka 70 tangu azaliwe Septemba 14, 1955, jijini Chicago, Marekani.

Papa Leo XIV, ambaye alichaguliwa kuwa Khalifa wa 267 wa Kiti cha Mtakatifu Petro Mei 8, 2025, ameadhimisha kumbukumbu hiyo muhimu huku akipokea baraka na pongezi kutoka kwa waumini wa Kanisa Katoliki duniani kote.

Safari yake ya huduma takatifu ilianza Juni 19, 1982 alipopewa daraja la Upadre, na baadaye Juni 12, 2014 akapandishwa katika daraja la Uaskofu. Septemba 30, 2023, akiwa miongoni mwa Makardinali 21 walioundwa na Papa Francis, aliendelea kuimarisha nafasi yake katika uongozi wa Kanisa.

Waumini wa Kanisa Katoliki duniani wameungana kumtakia afya njema, maisha marefu na baraka tele katika majukumu yake ya kuongoza zaidi ya waumini bilioni moja wa Kanisa Katoliki.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: