Benki ya Exim Tanzania imefanya tamasha linalojulikana kama ‘Exim Bima Festival 2024’ lenye lengo la kuchangia huduma za afya hususani kwa Wagonjwa wenye changamoto ya Afya ya Akili.

Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amezindua Tamasha la Exim Bima Festival ikiwa na kaulimbiu ‘Amsha Matumaini’, ambalo lengo ni kurudisha kwa jamii ambapo imeshafanya hivyo na kuchangia kiasi cha shilingi milioni mia tatu kwa muda wa miaka mitano ili kurudisha kwa jamiii na kiasi hicho safari hii kitapelekwa kwa wagonjwa wenye changamoto ya afya ya akili.

Akizungumza na wanahabari katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam lilipofanyika tamasha hilo, Waziri Kikwete ambaye alimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassimu Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, amesema kuwa fedha zinazopatikana zinakwenda kuchangia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwenye wenzetu wenye tatizo la afya ya akili.

“Ninatoa wito kwa makampuni na taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya Exim. Suala la Afya ya akili lazima lipewe kipaumbele na kila mtu, sio jambo la serikali au wizara ya afya tu, bali pia makampuni, mashirika, wadau wa maendeleo, na jamii kwa ujumla. Kwa pamoja, tunaweza kuunda mfumo bora wa afya unaojumuisha kila mtu na kuhakikisha kuwa hakuna anayeachwa nyuma,” anasema Mhe. Ridhiwani.


Waziri Kikwete akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kuzindua tamasha hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu akizungumza na wanahabari kwenye tamasha hilo amesema "Tumekuja kusapoti na kuunga mkono sisi kama Serikali tuko pamoja nao kuhakikisha kwamba jambo hili linafanikiwa".

Kwa upande Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu amesema wao kwao utamaduni wa kurejesha kwa jamii wanachokipata ni wa kamawida na wamesha fanya mambo mbalimbali kama kuchangia damu, kuchangia madawati kwa shule mbalimbali.

Hivyo kwa mwaka huu wao na makampuni mengine ya bima wameona waje na Tamasha la Exim Bima kwaajili ya kuwachangia watu wenye afya ya akili kwa kuwa changamoto hiyo kwasasa imeonekana kuwa kubwa hivyo wao watahakikisha wanaendelea kusaidia ili kupunguza tatizo hilo au kulimaliza kabisa.



Waziri Kikwete (kulia) akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Exim Bank, Jaffari Matundu.

---
“Siku ya leo tumekusanyika hapa kwa ajili ya suala la afya ambapo tumelenga kuwasaidia Watanzania wenzetu wanaokumbwa na tatizo la afya ya akili. Takwimu zinaonyesha tatizo la afya ya akili limekuwa mtambuka na hatari zaidi ni kuwa kundi lililoathirika zaidi ni la watu wenye umri wa kati ya miaka 15 na 39 ambao ndio nguvu kazi ya taifa,” anasema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw. Jaffari Matundu.

Katika jumla ya mikoa 28 nchini, mikoa mitano tu ndiyo ina vituo vinavyotoa huduma za afya ya akili zinazokidhi viwango. Ukubwa na hatari ya tatizo hili ni takwimu kuonesha kuwa kundi lililoathirika zaidi ni la wenye umri wa kati ya miaka 15 na 39 ambao ndio nguvu kazi ta taifa na hivyo kuhitajika juhudi za ziada kuokoa kizazi hiki kwa ajili ya ustawi na maendeleo ta Tanzania.

Exim Bima Festival 2024 ni moja ya malengo ya mpango wa ‘Exim Cares’ wa Exim Bank Tanzania. Tamasha la mwaka huu limepanga kuelekeza nguvu zake katika kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa wa bima katika jamii yetu huku likijikita katika kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma za afya ya akili na ustawi wa jamii ya Watanzania kote nchini. Benki ya Exim imejiwekea lengo la kukusanya jumla ya TZS milioni 300 ndani ya miaka mitatu ijayo ili kugharamia huduma muhimu na maboresho ya miundombinu katika vituo vya afya ya akili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: