Wapenzi wa mchezo wa mpira wa kikapu wakishuhudia baadhi ya timu zilizoshiriki  bonanza hilo zikichuana leo kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga 
ambalo lilikuwa na msisimuko mkubwa likiwakutanisha mamia ya wananchi  kutoka maeneo mbalimbali Jijini Tanga


TIMU
za mpira wa Pete (netball) za Bandari na Jiji zikichuano katika bonanza
hilo ambapo kwenye mchezo huo,Jiji iliweza kuibuka na ushindi wa  mabao
30-1 dhidi ya wapinzania wao ambapo kipindi cha kwanza Jiji iliweza
kuongoza kwa mabao 18-0 dhidi ya Bandari
Wachezajji
wakichuana katika mechi ya mpira wa pete kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani
mjini Tanga leo katika bonanza la michezo ambalo limeandaliwa na Radio
ya TK FM kwa kudhaminiwa na Tanga City Lounge,Tanga Fresh,Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF),Vodacom,Amic Design,Chuo cha
Utumishi wa Umma(TPSC) Tawi la Tanga,Katani Limited,Leen Events
Planner,Shirika la Maendeleo la BRAC Tanzania,Jaysen Studio 
Wananchi wa mkoa wa Tanga wakishuhudia uhondo wa michezo mbalimbali katika bonanza hilo
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya chuo cha Utumishi Mkoani Tanga wakitoka uwanjani mara baada ya mechi yao kumalizika
Wachezaji
wa timu ya Maveterani ya Tanga Middle Age wakipasha kabla ya kuwavaa
wapinzani wao Kilombero Veterani ambapo Tanga Middle Age walishinda kwa
bao 1-0


Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akitoa elimu kwa mkazi
wa Jiji la Tanga aliyetembelea banda lao waliloweka kwenye bonanza hilo
kwa lengo la kuhamasisha jamii kujiunga na mfuko huo ili kuweza
kunufaika na matibabu

Wachezaji wa timu za maveterani
wakichuana katika Bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake kwenye
uwanja wa CCM Mkwakwani Mjini Tanga ambalo liliandaliwa na kituo cha
Radio cha Jijini Tanga (TK)


Mashabiki wa michezo wakifuatilia kwa umakini bonanza hilo

Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya Mkoani Tanga (NHIF) Denis Kapinga akitolea ufafanuzi baadhi ya
huduma wanazozitoa wakati wa bonanza hilo


Msimamizi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga,Dinna Mlwilo
kushoto akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika kwenye banda lao leo
kwenye bonanza la Michezo ambalo lilifanyika kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani mjini Tanga
Wafanyakazi wa Radio TK FM ya Jijini Tanga kushoto
ni Mamy Mohamed ambaye ni Meneja wa Kituo hicho kulia ni George Kivumbi
ambaye ni Program Manager katikati ni DJ Rogger Kiss wakiwa katika
bonanza hilo
 Mamy Mohamed ambaye ni Meneja wa
Kituo cha Radio cha TK FM ya Jijini Tanga akitoa utaratibu wa zawadi kwa
washindi mara baada ya kumalizika bonanza hilo
Mkuu
wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akiwa na
Mkurugenzi wa Radio TK ya Jijini Tanga,Saidi Othumani kushoto wakati
alipokwenda kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katika
Bonanza hilo
 Mkurugenzi wa Radio TK ya Jijini Tanga,Saidi Othumani kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
 Ally Choki mzee wa Farasi kulia
akiwa na Luiza Mbutu kwenye jukwaa wakitumbuiza katika Bonanza la
Michezo ambao liliandaliwa na Radio TK FM ya Jijini Tanga
 Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
 Wasanii wanaounda Bendi ya Twanga Pepeta wakitumbuiza Jukwaani
 Baadhi ya washiriki  waliojitokeza katika bonanza hilo wakipiga picha ya pamoja

  Baadhi ya washiriki  waliojitokeza katika bonanza hilo wakipiga picha ya pamoja
Wananchi wakifuatilia Bonanza hilo

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: