Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza hii leo, Julai 04,2016 katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Samwel Sweda, akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Ilmela, Mhe.Dkt.Leonard Moses Masale (kushoto) akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (katikati).
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe.Mary Onesmo Tesha, akiapa hii leo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kushoto)
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Mhe.Mtemi Msafiri Simion (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (katikati).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, CP. Clodwin Mtweve, akizungumza katika hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza iliyofanyika hii leo katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Sala kutoka kwa Sheikh mkuu wa Bakwata mkoani Mwanza, kabla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za mkoa wa Mwanza.
Sala kutoka kwa Kiongozi wa Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza, kabla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za mkoa wa Mwanza.
Afisa Habari na Mahusiano kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na Siasa mkoani Mwanza
Viongozi wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Viongozi wa dini mkoani Mwanza, wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Baadhi ya viongozi kutoka kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakifuatilia zoezi la kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza
Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, wa nne waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza (waliosimama nyuma) na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza.
---
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015- 2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwenye wilaya walizo pangiwa.

Akizungumza baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.

Mkuu huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na kukomesha Utumiaji wa dawa zakulevya.

Aidha ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti mosi, suala la wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.

Mongella amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata ivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara.

Walio apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26, Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.

Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa habari na Mahusiano
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
MWANZA.
04, Julai, 2016.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: