Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akipekua mafaili ya hukumu
za migogoro ya ardhi ili kujiridhisha kama haki inatendeka kwa wananchi
wakati alipotembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akiongea na watendaji wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
Baadhi ya watendaji na watumishi wa umma wakimsikiliza Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula
katika ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini.
---
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ayataka Mabaraza ya Ardhi na Nyumba kuepuka rushwa kutoka kwa wenye fedha ili kuwapa upendeleo na kukandamiza wanyonge katika maamuzi yahusuyo migogoro ya ardhi.
Mheshimiwa Mabula ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea Baraza la Ardhi na Nyumba la Tanga mjini. Wakati wa ziara hiyo Mhe. Naibu Waziri amepiga marufuku tabia ya baadhi ya watu ambao huwapa pesa waendesha mashtaka na wenyeviti wa mabaraza ya Ardhi na nyumba ili kupindisha sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments: