Evance Luvinga |
Mnisamehe bure leo nimeamua kubadili pombe nyingine maana ile nzanzi inanilewesha sanaaaa mpaka nawauzi watu kwa maneno yangu yasiyofikirika zaidi...leo nimeamini komoni ni tamu sana na inalewesha taratibu sanaaaa ukizidiwa unalala..
Leo tuanze na SIASA nchini.
1809-1865 US PRESIDENT ABRAHAM LINCOLIN aliwahi define a democracy, "A government of people,by the people,for the people" Maana yake ni nini?ni "Serikali ya watu,iliyowekwa na watu,kwa ajili ya watu" Rais wetu mpendwa anasema tusifanye siasa Mpaka 2020 maana yake ni nini, kwamba watu wasisikie tena kitu kinachoitwa democracy tena kuweka mipaka wakati watu hao ndio wamewaweka madarakani. Tumempinga babu yetu Abraham Lincolin, tumempinga babu yetu Nyerere alivyoleta vyama vingi nchini.
Leo wabunge wa upinzani nchini marekani wamegomea serikali yao kwa kukaa chini kwasababu ya kudhibiti silaha nchini mwao, leo UKAWA wanatolewa bungeni kwa nguvu kisa wanaikosoa serikali yao....mmmmmmm hii komoni ya leo noma.
Eti Mtu asipodai risiti ya mia tano anaikosesha serikali shilingi mia moja mnamfunga miaka mitatu mnamhudumia malazi chakula na matibabu. Fisadi anaibia serilkali bilioni 2 mnamfunga miaka miwili.
Naomba kuuliza nikitoa hela ATM alafu nisipodai risiti pia naenda jela? Kuna haja ya kuongeza magereza ya kutosha maana wengi tunahusika apa.
Sinywi tena komoni ya leo...
AJIRA:
Leo Rais ametangaza kutoajiri mfanyakazi yoyote mpya serikalini.
sasa najiuliza na pombe zangu hizi hivi itakuaje kwa wale wanafunzi vyuoni waaodaiwa mikopo yao? Watalipaje? Kujiajiri wenyewe wanahitaji mtaji, je! Wanatoa wapi?
Kuwa na serikali ni jambo moja ila kutawala nalo ni jambo jingine.
Hii pombe sinywi tena maana nawaza ujinga tu apa.
MICHEZO
Eti leo Yanga awajalipwa fedha zao za FA Cup mmmmm wakipigiwa TFF wanasema wawafwate ofisini wakienda wanawapiga danadana YANGA wakaenda mbele zaidi kuwafwata wazamini yaanai TBL wakawaambia waende TFF. Yaani ni danadana zaidi.ya zile za Ronaldo sasa YANGA wameamua kwenda kwenye vyombo vya habari eti TFF wanarudi tena kuwaambia YANGA wasiwaseme kwenye media, heeeee sasa si muwalipe kama amtaki kutangazwa kwenye media????
•Natangaza kuanzia leo hii komoni sinywi tenaaaaaa Naona imeanza kunipanda kichwani.
KUZALIWA HAKUKUA CHAGUO LETU,WALA KUFA HAKUKUA CHAGUO LETU PIA, ISIPOKUA TUNAWEZA KUCHAGUA NAMNA YA KUISHI.
MUNGU AKUPI UNACHOTAKA, MUNGU ANAKUPA UNACHOSTAHILI.
UKAWA huu ndio muda wa kukaza misuli na mkanda zaidi kwani ufalme wa MUNGU ndio unakaribia.
©Ngoja nisubiri ujio wa PAULO KAGAME nchini July mosi.
Naweza kunywa Mbege maana komoni ni shidaaaaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: