Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake
lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu
jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo
la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer (kulia) akiendelea na zoezi la
kuhakiki Silaha za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiitoa silaha yake aina Bastola kwa ajili ya uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon
Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya
uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka vizuri silaha yake aina ya Shortgun mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kuhakiki silaha
zake Ikulu jijini Dar es Salaam. Mheshimiwa Rais amewataka wananchi wote
wanaomiliki silaha kujitokeza kuhakiki silaha zao kama alivyoagiza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiweka vizuri silaha yake mezani kwa ajili ya uhakiki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka dole gumba katika moja ya fomu za uhakiki Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.














Toa Maoni Yako:
0 comments: