Wanafamilia wa Marehemu Sarah Dumba wakionesha sura za huzuni na Majonzi baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
Vijana wa Scauti wakiwa wamebeba jeneza lililohifadhi mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Marehemu Bi. Sarah Dumba mara baada ya kuwasili nje ya viwanja vya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Rosemary Staki pamoja na Wakuu wa Wilaya kutoka Wilaya mbalimbali wakiongozana na vijana wa Scauti waliobeba mashada kuelekea kanisani tayari kwa ibada.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria kwenye ibada ya kumuaga Marehemu Sarah Dumba.
Viongozi wa dini wakiongozwa na Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoa wa Njombe Askofu Isaya Japhet Malenge wakiombea dua mwili wa marehemu.
Msafara uliobeba Mwili wa marehemu Sarah Dumba umeondoka leo saa tisa alasiri kuelekea Dar es Salaam ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwake Kigamboni.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE AMINA.


Toa Maoni Yako:
0 comments: