
Kasendeka, mhanga wa ajali iliyohusisha pikipiki mbili maarufu kama bodaboda eneo ilipo Club Royal karibu na lango kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi cha Tabora zamani kikifaahamika kama UHAZILI.
Kamera
ya mtandao huu imelimulika tukio baya la ajari iliyohusisha pikipiki
mbili eneo la Club Royal karibu na lango la kuingilia chuo cha Utumishi
wa Umma cha Tabora zamani UHAZILI.
Mfuatiliaji
wa tukio alibainisha dereva mmoja alikuwa anatokwa na harufu ya pombe
kitu kilichodhihirisha kuwa alikuwa amelewa huku kamchukua abiria na
akiendesha chombo cha moto.
Mashuhuda
waliuambia mtandao huu kuwa wanalalamikia jeshi la polisi kuto
kujitokeza mapema eneo la tukio licha ya kuwa hapana umbali unaozidi
mita 100 kutoka eneo la tukio, mfuatiliaji wa tukio aliwahoji kama kuna
yeyote aliyetoa taarifa kituoni dhidi ya tukio hilo lakini hakupata
majibu.
Kasendeka akiwa anazinduka ziduka, akili inakuja baada ya kuzimia kwa muda kidogo kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki mbili eneo la Club Royal karibu na lango/ geti la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI.

Abiria na mhanga wa ajali hiyo akiwa anaugulia maumivu baada ya ajali iliyotokea muda mfupi maeneo ya Club Royal karibu na geti kuu la kuingilia Chuo Cha Utumishi wa Umma zamani UHAZILI



Mashuhuda wa tukio la ajali iliyohusisha pikipiki mbili maeneo ya Club Royal

Kasendeka akiwa anaangalia pikipiki yake baada ya ajali hiyo muda mfupi alipozinduka.

Askari wa Jeshi la usalama barabarani akijongea eneo la tukio. Inakadiriwa ni zaidi ya dakika 15 au zaidi (Kwa mujibu wa mashuhuda) zilipita ndipo askari alijitokeza eneo la tukio licha ya tukio hilo kutokea umbali wa mita za makadirio zisizozidi 100 kutoka kituo kukuu cha Polisi mjini Tabora.

Askari akifuatilia tukio hilo baada ya dakika zinazokadiriwa na mashuhuda wa tukio kuwa ni zaidi ya 15 toka ajari imetokea.

Askari akimhoji Kasendeka kabla ya kwenda naye kituoni huku mhanga mmojawapo kuwa tayari alishakimbia eneo la tukio na kuisaliti pikipiki eneo la tukio.

Picha na Aloyson.




Toa Maoni Yako:
0 comments: