Na Sylvester Raphael
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa
Papa nchini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla atembelea mkoa wa
Kagera katika ziara ya kujione shughuli mbalimbali za Kanisa Katoliki
mkoani zinavyotekelezwa pia na kutoa Baraka za pamoja kwa wakristo wa
kanisa hilo.
Balozi Padilla akiwa ofisini kwa Mkuu wa
Mkoa Kagera alipowasili kumsalimia aliishukuru serikali ya mkoa wa
Kagera kwa kuwaunganisha wananchi wa Kagera bila kujali imani zao
ambapo wanafanya shughuli zao kila mmoja kwa imani yake bila usumbufu
wowote
Pia Balozi Padilla alisema kuwa serikali inafanya kazi moja ya
kuwaudumia wananchi pia na dini zinafanya kazi ya kuwahudumia wananchi
hao hao kiroho kwa hiyo hakuna haja ya serikali na dini kugombana wala
kukwaruzana kwasababu wote wanafanya kazi moja kwa wananchi.
“Ni
bora kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya serikali na dini na
nashukuru jambo hilo linatekelezwa mkoani Kagera, nimekuja kukagua
shughuli mbalimbali hapa na kupata baraka za pamoja na wakristo wa mkoa
wa Kagera ili kujenga jamii moja yenye familia moja katika kumtukuza
Mungu.” Alimalizia Balozi Padilla.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera John Mongella akimkaribisha Balozi Padilla
alimshukuru kwa kufanya ziara mkoani Kagera na alimweleza kuwa serikali
inatambua juhudi za kanisa Katoliki katika kuleta maendeleo kwa wananchi
hasa ujenzi wa shule na hospitali kama huduma za jamii kwa wananch,i
pia kutoa huduma za kiroho zinazosaidia kukuza maadili katika jamii.
Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa chini Tanzania, Francisco Montecillo Padilla ziara yake imeanza leo Septemba 3, 2015 na anatarajia kuwepo mkoani hapa kwa takribani siku sita, aidha Balozi Padilla anatarajiwa kuongoza ibada takatifu ya maombezi ya Bikra Maria katika hija huko Nyakijooga Parokiani Mugana Wilayani Missenyi tarehe 6.09.2015 siku ya Jumapili.


Toa Maoni Yako:
0 comments: