Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert  Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel.
---
Habari na libeneke la kaskazini blog.

Tamasha la 10 la vyombo vya habari  na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo  timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.

Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha
Media. mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.


"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema


Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.


Rutaraka alisema kampuni yao kwa miaka mitano sasa inadhamini tamasha hilo na wanajivunia mafanikio makubwa.


Tamasha hilo, limedhaminiwa na kampuni ya bia nchini(TBL) Kampuni ya Mega Trade, Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Shirika la Nyumba nchini
(NHC) Kampuni ya SBC(T) Ltd,Mamlaka hifadhi Ngorongoro(NCAA), Taasisi
ya FAIDIKA na Tanzanite One.

Makamu Mwenyekiti wa TASWA Arusha, Adrea Ngobole alisema wadhamini wengine wa Tamasha hilo watatangazwa karibuni sambamba na zawadi na mgeni rasmi.
 Meneja wa masoko na mauzo wa Kampuni ya SBC (T) Lalit Sharma, akimkabidhi mipira Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha, Mussa Juma kwa ajili ya Tamasha la kumi la waandishi wa habari mkoa wa Arusha,Manyara na Dar es Salaam na wadau wa habari, ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa Sheikh Amri
Abeid.

 Makamu
Mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha,Andrea Ngobole, akipokea
vikombe kutoka kwa Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa
FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay jana Palace
Hotel  kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na ambalo
litashirikisha pia wafanyakazi wa taasisi hiyo, ambalo litafanyika
Augost 29 uwanja wa Sheikh Amri Abeid



Wadhamini na viongozi wa TASWA Arusha, wakiwa kwenye
kikao na waandishi wa habari kuelezea Bonanza la vyombo vya habari na
wadau wa habari mkoa wa Arusha,ambalo litafanyika Augosti 29 uwanja wa
Sheikh Amri Abeid.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: