Meneja wa baa ya Safari resort Kimara Bw. Robert Herman akielezea furaha
yake baada ya baa yake kutembelewa na promosheni ya Tusker Fanyakweli
Kiwanjani huku akifafanua kuwa kiwanja hicho kilichopo Kimara jijini Dar
es salaam ni mahali tulivu sana kwa wateja. Baa hiyo iliibuka mshindi
wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya
Tusker.
Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G.
Habash akielezea utaratibu wa utoaji zawadi kwa wapenzi wa bia ya Tusker
waliofika katika baa ya Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo iliyopo
Tandika jijini Dar es salaam. Baa hiyo ilibuka mshindi wa wiki kwenye
kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo
likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli
pale wanapotoa huduma kwa wateja.
Mkazi wa Mwembeyanga Bw. Frank Kabisi (katikati) akifurahia zawadi yake
ya mfuko na Tisheti alizopewa wakati wa wa hafla ya kuipongeza baa ya
Kisuma iliyopo Mwembeyanga Tandika mara baada ya baa hiyo kuibuka
mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani
inayoendeshwa na bia ya Tusker toka kampuni ya bia ya Serengeti.
(Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani na
Tusker Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica
Mbilinyi.
Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Bw.
Victor Mhindi akikabidhi zawadi ya polo shirt kwa Papaa Mazengo mkazi wa
Kimara wakati wa promosheni ya Fanyakweli kiwanjani katika baa ya
Safari resort. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa shindano hilo baada
ya kupigiwa kura na wateja wa baa hiyo. (Kushoto) ni mshereheshaji wa
promosheni hiyo Gadner G. Habash.
Mkazi wa Temeke Bi. Sikudhani Idd akituma salamu kwa marafiki zake
kupitia redio Efm iliyokuwa ikisikika moja kwa moja kwenye kiwanja cha
Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo ya Tandika jijini Dar es salaam
baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli
Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo lake likiwa ni
kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli pindi
wanapotoa huduma kwa wateja. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya
Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo
Bi. Veronica Mbilinyi.


Toa Maoni Yako:
0 comments: