→☆Mheshimiwa spika kwanza naomba uelewe nampenda sana Diamond siwezi kumuacha, Zari yeye anapoteza tu muda.
La pili mheshimiwa spika ni kuhusu kajala yote ninamuachia Mungu maana limtolea milioni 12 asifungwe ila mwisho wa siku akanichukulia bwana angu.
~~Na mwisho kabisa mheshimiwa spika naomba kuunga mkono hoja na ninarudia tena na tena nampenda sana Diamond.
MAKOFI TOKA KWA WABUNGE... wawawawa..... wawawawawa... wawawawawawa.
SPIKA:Ahsante mrembo wa bunge na mimi naahidi kukusaidia kutia fitina mpaka tuhakikishe ZARI anaachika.
Tunaendelea waheshimiwa wabunge na sasa namuita mheshiwa Juma Nature mbuge kutoka KIUMENI TEMEKE.
Juma Nature: Mheshimiwa spika kweli mbunge mwenzetu kuporwa boyfriend wake na Zari imeniuma sana, yaani kigheto ghetto tunasema kapigwa tatu bila, naomba serikali tukufu ilivalie njuga hili swala.
Spika: Nimekusikiliza Juma Nature kwanza pole sana umeongea kwa hisia imenifanya nikumbuke hujuma ulizokuwa unafanyiwa kwenye show zako, ila tuendelee kwanza na hoja iliyopo namwona pale mheshimiwa Afande Sele.
Afande Sele: Ahsante mheshimiwa spika kunipa nafasi, nimewaza sana kweli dunia ina mambo toka kitambo, nimeumia sana kijana wetu Diamond na Alikiba wakiwa na bifu ila hili swala la Diamond kwenda kwa Zari na kumwacha mheshimiwa Wema imeniuma sana (anaongea kwa hisia mpaka anavua suruali).
Wabunge wanashangilia na kugonga meza kwa nguvu kwaaa kwa kwaaa kwaaa vua tuone.



Toa Maoni Yako:
0 comments: