Kikosi kazi cha Watumishi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC) wakiwa tayari kutoa huduma kwa wageni mbalimbali watakaotembelea banda hilo katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Athuman Bakari, Aziza Tamim na Debora Mligo.
Watumishi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA-CCC)wakitoa huduma kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda hilo leo.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC), Hamza Johari akizungumza jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari waliotembelea banda hilo.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC), Hamza Johari akiwa katika mahojiano na waandishi wa habari wa Magazeti ya serikali(Daily News na Habarileo) waliotembelea banda hilo Dar es Salaam jana.
 Debora Mligo na Aziza Tamim wa TCAA-CCC wakiwasikiliza wageni waliotembelea banda hilo.

Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za 
Usafiri wa anga (TCAA-CCC) liliopo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa 
Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo. Kutoka 
kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza Hamza Johari, 
waelimishaji na wahamasishaji wa baraza hilo Debora Mligo na Athuman Bakari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Charles Chacha (mwenye suti) katikati akiwa katika picha na ya Pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Ushauri la watumiaji Huduma za Usafiri wa anga (TCAA-CCC) wakati alipotembelea kwenye banda lhilo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: