Mpishi Mkuu wa Bar ya Tumaini ya jijini Mbeya, John Mushi(kushoto) akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 yaliyofanyika katika Chuo cha uhasibu(TIA) mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela.
Katibu Tawala wa jiji la Mbeya, Quip Mbeyela(katikati) akimkabithi mshindi wa Safari Nyama Choma 2015, John Mushi kitita cha Shilingi 1,000 000/= mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano hayo yaliyofanyika katika Chuo cha TIA mwishoni mwa wiki.
Mpishi Mkuu wa Bar ya Tumaini ya jijini Mbeya, John Mushi(kushoto) akiaonyesha kitita cha pesa tasliomu Shilingi 1,000 000/= mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 yaliyofanyika katika Chuo cha uhasibu(TIA) mwishoni mwa wiki.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lger, Edith Bebwa na Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela.

TUMAINI Bar jijini Mbeya wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Chuo cha Uhasibu(TIA) Mbeya na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.

Akizungumza na wakazi Mkoa wa Mbeya waliohudhuria mashindano hayo,Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Quip Mbeyela aliwashukuru kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kwa kuendelea kudhamini mashindano ya Nyama Choma yenye mvuto wa pekee ambayo yanawapa picha halisi wakazi wa Mbeya kuwa wapi wanaweza kupata nyama choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika jiji la Mbeya.

Alisema Mbeyela kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbali mbali za jijini Mbeya ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo na sisi kama Serikali tuko pamoja nanyi.

Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mbeya na mwisho aliwapongeza mabingwa wapya Tumaini Bar kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015, Tumaini Bar na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mbeya waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 jijini Meya.

Mwisho Edith aliwaomba washiriki wote ambao walipata zawadi wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashndano yajayo ya 2016.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: