Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa.
Bondia Thomas Mashali akipima uzito
Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kulia ni mpinzani wake Said Mbelwaakishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa.
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kulia ni mpinzani wake Japhert Kaseba akishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa.
Mabondia Said Mbelwa na Japhert Kaseba wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa.
Bondia Abdallah Pazi Akipima uzito
---
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Mada Maugo na Kalama Nyilawila nusula wazipige kavu kavu wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa wakati wa upimaji uzito

Maugo alienda kumtambia Kalama na kumpiga kibao pamoja na teke kali sana lililompiga Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiamulizia ugomvi uho hapo ndipo lilipozuka songombingo kali kwa mashabiki wa kambi zote mbili wakitaka kuzipiga kavu kavu uku maugo akiwa ameshapanda moli wa kupigana nje ya uringo

Mpambano uho ambao utakuwa na michezo mingine ya kumaliza ubishi ni kati ya Thomas Mashali atakaemkabili Abdallah Pazi na Japhert Kaseba atapambana na Saidi Mbelwa mipambano hiyo yote yatafanyika siku ya jumapili march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa ambapo baadhi ya mashabiki wameomba baadhi ya daladala zinazofanya kazi usiku kwenda kuwa chukuwa pindi wamalizapo kuangalia mapambano hayo yaliyo na ushindani wa kweli
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: