Kaimu Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania Cecile Tiano (kulia) akiongea na waandishi habari mkoani Arusha (hawapo pichani), wakati kutangaza kuongeza uwekezaji dola milioni 30 kwa mikoa ya kanda ya kaskazini mwishoni mwa wiki, kulia kwake meneja mkuu kanda hiyo Bw. David Charles.

Na Mwandishi Wetu.

Kaimu Meneja mkuu waTigo Tanzania, Cecile Tiano, ameelezea nia ya kampuni yake kuongeza uwekezaji katika mikoa ya kanda ya kaskazini kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 30 alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Arusha.

Tiano, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi huu, ameisifu kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Dodoma na Kilimanjaro kuwa ni eneo la kibiashara na utalii bila kusahau kuwa ni njia kuu ya kuelekea mataifa jirani.

Alifafanua kwamba Tigo ina jumla  ya minara 334 katika ukanda wa kaskazini ikiwemo 71 iliyojengwa mwaka 2014. Mwaka jana Tigo ilijenga jumla ya minara 312 nchi nzima.

“Mwaka huu tumepanga kujenga minara mingine 748 nchi nzima ambayo 300 itakuwa katika kanda ya kaskazini ilikuhakikisha wakazi wa vijiji vya mikoa yote mitano wanaunganishwa na huduma zetu. Kwa wastani wa dola 100,000 kila mnara, hii inamaanisha uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 75 nchi nzima ikiwemo dola milioni 30 katika mikoa hii mitano.," Alisema.

“Hii inamaanisha watu wengi zaidi watapata fursa mpya za kijamii na kiuchumi, wakiunganishwa katika uchumi wa kidunia kupitia mtandao wa intaneti – na kwa kufanya hivyo tunawawezesha kujiunga na mfumo mpya wa digital,” alisisitiza Tiano.

Kanda ya Kaskazini pia imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na mipango kadha ya udhamini na miradi ya kijamii kutoka Tigo, miradi ambayo Tiano alisema ina lengo la kuleta mageuzi chanya katika nyanja za elimu, afya, mazingira, ujasiriamali (ajira), sanaa na michezo.

“Kupitia juhudi zetu kama zile zama shindano ya Tigo Ngorongoro Run, mbio ambazo zimekuwa zikifanyika Karatu kila mwaka, kampuni yetu, pamoja na wadau wengine, tumeweza kukusanya fedha ambazo hutumika kununulia vya ndarua shuleni, vifaa vya hopitali mbalimbali katika wilaya ya Karatu,” alisema.

Katika hatua nyingine Tiano ametangaza udhamini wa Tigo kwa mbio za marathoni za Kilimnajaro mwaka huu kwa kiasi cha shilingi milioni 80. Mbio hizo zitafanyika tarehe 1 Machi 2015 ambapo Tigo inadhamini nusu marathoni ya kilomita 21, alisema.

“Sababu ya Tigo kujiingiza katika mashindano haya nikuonesha nia yake ya kuendeleza sekta ya michezo na nyanja nyingine za kijamii na za kiuchumi katika nchi hii, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Tigo imekuwa ikiwekeza kwenye miundo mbinu yake kwa wastani wa dola milioni mbili kwa wiki nchi nzima. Uwekezaji huu, kwa mujibu wa Tiano, umesaidia kupanua mtandao wake mpaka sehemu za vijijini; kuboresha mtandao wake hadi kufikia vipimo vya 3G hivyo kuwawezesha wateja kupata huduma ya Internet; kuelimisha wafanyakazi wake na kuleta manufaa kwa jamii kwa kuwekea katika miradi ya kijamii
.
Tiano aliendelea kusema kuwanda niya miezi 12 iliyopita Tigo imekuwa kampuni ya kwanza kubuni huduma mpya zikiwemo kutuma na kupokea pesa kutoka Rwanda kupitia Tigo Pesa; kuanzisha huduma ya bure ya Facebook kwa Kiswahili pamoja;na kuanzisha ushirikiano na kampuni nyingine za simu nchini kuwawezesha wateja kutuma au kupokea pesa kutoka mitandao hiyo. Mafanikio mengine ni kuwawezesha wateja wake kuwekea na kutoa pesa kutoka akaunti zao za benki kupitia simu zao za mkononi; kuwapa wateja gawio la faida itokanyo na utunzaji fedha zao katika akaunti zao za Tigo Pesa; na hivi karibuni uzinduzi wa huduma ya Tigo music inayowapa wateja wake fursa ya kufurahia muziki bila kikomo kupitia Deezer.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: