Mke alimuaga mume wake anaenda kumsalimia mam yake mgonjwa kijijini, akaondoka ijumaa na kurudi jumatatu huku akiwa na matunda kibao pamoja na vyakula vingine toka huko kijijini akisema ni mama amenipa kwa ajili yako mume wangu na watoto.

Mume akamuuliza kwa upoooole...

Mama anaendeleaje!

Mke akajibu kuwa amempeleka hospitali ila anaendelea vyema.

Mke aliongezea kwamba;

Mama yake amemsisitiza amtembelee tena baada ya siku chache akae huko naye wiki.

Mke akaendelea kusema; nina hofu na afya ya Mama. Aliyasema hayo kwa uchungu huku machozi yanamtoka.

Mume akamjibu kwa huruma atapona mpenzi usijali.

Mume akamwambia mke wake kwa hekima:

...ingiza vitu ulivyoleta jikoni.

Mke ile anaingia jikoni akamkuta mama yake mzazi aliyedai kaenda kumsalimia kijijini akiandaa chakula jikoni.

Kumbe mama yake alikuja kumtembelea pale tangu ijumaa yeye alivyoondoka.

Mke akabaki ameduwaa mlangoni mwa jiko asijue apeleke vitu jikoni au arudi sebuleni kwa mume wake.

Je afanyeje?
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: