Askari  wa FFU  wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana kama  njia ya  kulinda amani kwa  wafanyabiashara  ambao  waliendelea kutoa huduma  baada ya wenzao  kuwa katika mgomo.
MOja  kati  ya  maduka  mjini Iringa yakiendelea  kutoa  huduma  mbali ya wafanyabiashara  wengine  kuwepo katika mgomo  kushinikiza kuachiwa  huru kwa mwenyekiti wa  wafanyabiashara  Taifa  Bw  Johnson Minja.
Maduka  mtaa wa  uhindini mjini  Iringa  yakiwa  yamefungwa jana  kuunga mkono mgomo  wa wafanyabiashara  nchini.
Mmoja kati ya  wafanyabiashara  wadogo (machinga) mjini Iringa akiwa amepanga  bidhaa zake  nje ya  duka moja wao  eneo la Miyomboni kufuatilia wafanyabiashara  wenye maduka  kufunga maduka yao kushinikiza  jeshi la  polisi  kumwachia mwenyekiti  wao Taifa ,hapa  ni  kufa kufaana.
Wananchi mbalimbali  wa mji  wa Iringa  wakiwa katika  soko  kuu la mjini Iringa  kupata  huduma  zao wakati sehemu mbali mbali huduma zikiwa  zimesitishwa  kufuatia mgomo  wa wafanyabiashara  nchini.
Na matukiodaimaBlog.

BAADHI ya  wafanyabiashara   mkoani  Iringa  jana   wamegoma  kuungana na 

 wafanyabiashara    wenzao nchini  kushiriki mgomo  wa  kushinikiza jeshi la  polisi  kumwachia  huru mwenyekiti  wao  wa chama  cha wafanyabiashara  nchini Bw  Johnson  Minja anayedaiwa  kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.


Wafanyabiashara hao  waliosusia  mgomo  huo  walifikia uamuzi huo  kama  hatua ya  
kupinga uamuzi  wa  wenzao ambao walifunga maduka  yao kwa  siku nzima kuungana na  wafanyabiashara  wa  mkoa  wa Dar es Salaam  ambao walifanya   hivyo .

Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz  katika  mitaa mbali mbali  ya  mji wa Iringa na maeneo ya  nje ya  mji  wa Iringa ulionyesha  kuwa mgomo  huo kukosa ushirikiano  kutokana na baadhi ya maduka ya  pembezoni mwa  mji wa Iringa na yale ya  vijijini na baadhi ya maduka ya  katikati ya mji wa Iringa  kuendelea na huduma kama  kawaida huku  wakiomba  ulinzi kwa jeshi la  polisi  ili  wao kuendelea  kutoa  huduma kama  kawaida.

Huku cha kushangaza  hata  baadhi ya  salun na  bucha  za nyama katika baadhi ya maeneo mjini hapa  zilifungwa  huku baadhi ya maduka yanazozunguka  soko  kuu la Iringa  pia yakifungwa japo katika soko hilo umati mkubwa wa  wananchi  waliendelea kupata  huduma kama kawaida .

Mmoja kati ya  wafanyabiashara wa mji  wa Iringa Bw JOhn  sanga  alisema kuwa ameshindwa  kuungana na  wafanyabiashara  wa mji  wa Iringa katika mgomo  huo  kutokana na  shinikizo  kubwa ambalo  lilikuwa  likionyeshwa na watu  waliokuwa  wakisambaza  jumbe  za mgomo   huo  juzi na jana kupitia  kikundi  cha  watu kama 11  ambao   wengi  wao  walikuwa wakitoa  vitisho  wakati wa  kusambaza  taarifa   hizo.

"Kweli  nimeshindwa  kufunga duka  langu leo kutokana na vitisho vya watu hao ambao   wanatulazimisha  kufunga kwa nguvu huku  wakitambua kuwa  si kila mfanyabiashara  ni mwanachama  wa chama  chao   hicho cha  wafanyabiashara  ....kutulazimisha  kufunga  biashara  zetu ni kutunyanyasa  sisi tusio  wanachama na  tambua kila mmoja ana  maisha yake  wao badala ya  kukutana  viongozi kwa ajili ya  kulimaliza  suala hilo  wanataka  wote  tufunge  maduka  huu ni ushauri  mbaya  kuliko"

Hata hivyo  alisema  hajaweza  kufunga  na ataendelea  kutoa huduma  wakati wote wa mgomo  wa  wafanyabiashara  hao kwani  si  lazima  kila mfanyabiashara  kuungana nao katika  chama  chao na kiongozi  wao.

Huku mfanyabiashara  Geofrey   kalinga  akieleza  kusikitishwa na serikali kushindwa  kuchukua hatua kali kwa  kikundi hicho  cha wafanyabiashara   wachache ambao  wanachochea  mgomo huo na kuwakosesha wengine amani ya  kufungua  biashara  zao na  kuwa  kuendelea kuchelewa kuchukua hatua  ni kubariki migomo kama   hiyo  kuendelea.

Kwani alisema ni jambo la kushangaza  kuona watu hao  wachache wakitumia nguvu  kuwazuia  wengine  kuungana nao katika mgomo  huo huku wakitambua  kuwa  chama  hicho ni chama cha hiari  kujiunga ama kutojiunga  hivyo  walipaswa  kushughulika na  wanachama  wao na  sio wafanyabiashara   wote.

"Haya ni mambo ya ajabu sana hivi  inawezekana  vipi hiki  kikundi  cha wachache kutulazimisha  wafanyabiashara  wote  kujiunga na chama  chao... sasa leo wanatutaka  kufunga  biashara  kwa  muda  usiojulikana kesho  watakuja na  jambo   jingine lakini  swali la msingi hapa  hicho chama  chao kinatusaidia nini  sisi ambao  si  wanachama tunapofungiwa biashara zetu ya mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA) kwa  kuchelewa kulipa  kodi....ama  wanatusaidia   vipi na kodi  kubwa ya mapango ya  
vyumba  vya  biashara ambazo tumekuwa  tukilipa .....kama  jibu  hakuna
basi  watuache na  wao  waendelee na migomo yao"

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi  wafanyabiashara   waliofunga maduka  yao walisema  kuwa  sababu ya  kufunga maduka  kwa muda  usiofahamika ni kutoka  jeshi la  polisi  kumwachia huru kiongozi  wao kitaifa  Bw Minja anayedaiwa kukamatwa  toka  juzi na  jeshi  la polisi na hajulikani alipo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi  wa  mkoa wa Iringa Suzana Ndelwa  alisema  kuwa kufungwa kwa  maduka katika  mji  wa Iringa  kumewaathiri wananchi kiuchumi kutokana na baadhi yao  kutoka  nje ya  mji  wa Iringa kufuata huduma  za  jumla ila kufungwa kwa maduka  hayo kumeyumbisha  uchimi wao na  wa  Taifa kwa ujumla na  kuwa  ilipaswa kwa upande wa mkoa wa Iringa mkuu wa mkoa  huo kuingilia kati  suala hilo.

Mbali ya  baadhi yao  kutoma  kufunga maduka  yao  bado ule  usemi  wa kufa kufaana  ulionekana  kutawala katika maeneo mengi ya mji  wa Iringa kutokana na mgomo  huo baada ya  baadhi ya  wafanyabiashara  wadogo maarufu kama machinga  kunufaika  zaidi na mgomo  huo kwa  kupanga bidhaa  zao  nje ya maduka  yanayofanya  biashara  kama  zao na  kupata wateja  zaidi kupitia  mgomo  huo  huku baadhi ya  wafanyabiashara wakionekana  kuuzia  bidhaa  zao stoo na  wengine  kufungua maduka  yao nusu mlingoti na  kuendelea  kutoa  huduma kama kawaida.

Wakati wafanyabiashara  hao wakiwa katika mgomo huo mjini Iringa, Mafinga 
na  baadhi ya  wachache wa Ilula bado jeshi la polisi lilionekana
kuweka  ulinzi  wa  kutosha katika maeneo ya  wafanyabiashara hao
huku  askari  wa  kikosi  cha  kutuliza ghasia (FFU))  wakionekana 
kuzunguka  kila  kona ya  mji  wa Iringa  ili  kuthibiti vurugu  iwapo 
zingejitokeza.

Jitihada za  kumpata mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ama  kamanda wa  
polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan  Mungi ili kuweza  kuzungumzia 
jinsi mkoa ulivyojipanga kumaliza tatizo hilo la mgomo ama jeshi la 
polisi lilivyojipanga kuwalinda  wafanyabiashara  ambao  waligoma
kuungana na wenzao katika mgomo huo hazikuzaa matunda baada ya  simu 
za viongozi hao wawili kuita  bila  kupokelewa .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: