Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiwapungia mkono wafuasi wake mara baada ya Polisi kuyasambaratisha maandamano ya amani ya chama hicho yaliyokuwa na lengo la kuwakumbuka wanachama wenzao, walioteswa na kuuawa kwa kipigo cha Polisi huko Zanzibar Januari 27 mwaka 2001.
Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba (katikati) akiwa amewekewa ulinzi na wafuasi wa chama hicho wakati Polisi walipozuia maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike leo kuanzia Temeke Hospitali hadi Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam. (Na
Mpiga Picha Wetu)
Haki......
Walinzi maalum wa CUF wakiwa wameimarisha ulinzi katika gari alilopanda Mwenyekiti wa chama hicho.
Polisi wakizuia maandamano ya CUF katika eneo la Mtoni.
Mlinzi wa Prof. Ibrahim Lipumba akizozana na askari wa kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakati walipota kumkamata bosi wake.
Prof. Lipumba akiwa katika gari la Polisi
Mfuasi wa CUF akiwa chini ya ulinzi.
Prof. Lipumba akizungumza na maofuisa wa Polisi.

Prof. Lipumba akizungumza na maofuisa wa Polisi.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata wananchama wa Chama cha Wananchi CUF 32 akiwemo Mwenyekiti Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kwa kufanya maandamano ambayo si halali.

Awali polisi ilizuia maandamano yaliyokuwa yamepangwa na chama hicho ya kuadhimisha kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na mateso ya wananchi wa Zanzibar na Bara yalifanywa na vyombo vya usalama.

Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.

“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.

Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.

Siro alisema sababu kubwa ya kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuwa mwaka 2001 yalifanyika maandamano batili yaliyosababisha baadhi ya polisi na wananchi kufa.

“Jeshi la polisi likiruhusu hayo maandamano kuna uwezekano wa kutokea fujo na hayo maandamano ya mwaka 2001 yalikuwa si halali na kwenye maandamano hayo walikufa askari polisi,”alisema Siro.

Alisem sababu nyingine ya kuzuia maandamano hayo ni kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wanaojihusisha na mambo ya ugaidi hivyo kutokana na mazingira hayo jeshi la polisi linazuia mikusanyiko mikubwa kwa kuhofia kutokea mambo mabaya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: