Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kutoka kulia ni Mwakilirishi kutoka Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Doris Gweba, Diwani wa Kata ya Mchikichini Mhe.Riyani na Mgeni rasmi, Leopold Kaswezi.
Mgeni rasmi, Leopold Kaswezi (katikati), akizungumza na wahitimu hao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mchikichini, Mhe.Riyani na Mkurugenzi Mtendaji  wa Shirika lisilo la Kiserikali la Equality For Growth (EfG), Jane Magigita.
Mjumbe wa EfG, Emanuel Tuju akizungumza wakati akitoa shukurani kwa mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Bakari  Yusuph kutoka soko la Feri, akikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Batreti Malemula kutoka soko la Feri, akikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
 Soko la Ilala Boma Consolata.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Mwalimu Halima Kilimo kutoka soko la Buguruni kikabidhiwa cheti chake na mgeni rasmi.
Muhitimu wa mafunzo hayo, Mwalimu Chiku Hamisi kutoka soko la Buguruni, akionesha cheti chake kwa furaha baada ya kukabidhiwa.
Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.


Wahitimu wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wahitimu wakifuatilia matukio ya ufungaji wa mafunzo yao.

Hapa ni sebene tu kwa kwenda mbele wakifurahia kumaliza mafunzo hayo. 'Mbona wanyanyasaji katika masoko watakoma safari hii,  wahitimu 25 sio mchezo ni vizuri wajisalimishe mapema chezea sheria wewe'.
Hapa ni mduara na vyeti ni juu lazima mvione.
Wahitimu ya mafunzo ya usaidizi wa sheria katika masoko ya Manispaa ya Ilala wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayo ya siku 25, Mwanasheria wa Manispaa hiyo , Leopold Kaswezi (aliyevaa suti katikati waliokaa), aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na maofisa wa Shirika lisillo la kiserikali la Equality for Growth (EfG), kwenye sherehe zilizofanyika Hoteli ya Lamada Dar es Salaam jana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: