ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam. 

Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika.

Akizungumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

“Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta” alisema Luizer.

Aliongeza kwa kusema: "Hapa natetemeka siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Msiba uko Kigamboni maeneo ya Mikadi Beach.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: