1. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto Kabwe hakuniita ili kupata nafasi ya kujitetea, kutokana na shutuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwangu, kwamba nilipewa fedha kupitia akaunti ya Escrow.

2. Kujiuzulu sio fasheni, kwa kuwa fedha nilizopata ni kwa ajili ya mchango wa shule ya Barbro Johansson ya jijini Dar es Salaam na kujiuzulu ni kitu ambacho kina sababu zinazohitaji uwajibikaji. Nijiuzulu kwa kuwa nimepata mchango wa shule?

3. “Nijiuzulu kwa sababu gani?… kwa kupata mchango wa shule!… kujiuzulu ni kitu chenye sababu zake, kujiuzulu sio fasheni, lazima kuwe na sababu, hata Rais aliyenipa kazi atashangaa. Naona ufahari kufanikisha mchango wa shule yangu.
4. Aidha, serikali haijatamka kama James Rugemalira ana fedha haramu na kama fedha hizo, zikitajwa kuwa za haramu, shule yangu itazirudisha, kwa kuwa shule yangu haiwezi kupokea fedha iliyo haramu.

5. “Nilipostaafu kazi UN, Sweden waliniambia kuwa sasa naweza kuendelea kuomba mchango katika nchi yangu na ni kweli kwamba kadri taifa linavyokua wapo watu wenye uwezo na wanaoweza kuchangia katika masuala mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa ndio maana alianza kuomba michango kwa watu mbalimbali wakiwamo wa ndani ya nchi. Na kutokana na kuomba mchango, hata Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliwahi kutuchangia Sh milioni 278 kwa kuona umuhimu wa kuendeleza elimu ya mtoto wa kike na mwaka 2012, ndipo nilipomuomba mchango James Rugemalira kupitia kampuni yake ya Mabibo akiwa kama ndugu yake.

6. Nilipomwandikia Rugemalira, alinjibu nitachangiwa, lakini kwa masharti ya kwamba fedha hizo zipitie Benki ya Mkombozi. Na mimi sikuwa na akaunti katika benki hiyo na Februari 23 mwaka huu ndipo nilifungua na haukupita muda mwingi alinipigia na kuniambia kuwa tayari ameshachangia. Baada ya kupata mchango huo, niliwapigia viongozi wa Bodi ya shule kuwaeleza kwamba wamepata mchango `babu kubwa’ na alihamisha fedha hizo na kuzipeleka Benki M kwa ajili ya kulipa mikopo ya shule.

7. Profesa Tibaijuka anasema: “Nimejitolea maisha yangu kutafuta wafadhili kwani ada za shule hizo ni kubwa kwani ya Dar es Salaam ni Sh milioni nne na nusu na ile ya Bukoba ni Sh milioni mbili huku pakiwepo pia wanafunzi ambao hawalipi ada wakipatiwa ufadhili.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: