Na Mwandishi Wetu.

Jumla ya vijiji ni 9047 CCM imepata 7290 na Chadema 1248 Cuf 949 mitaa CCM Tanzania ipo 3740 CCM imepata 2116 Chadema 753 Cuf 235 hivyo CCM kwenye vijiji imeshinda kwa asilimia 80.58 Chadema 13.79 mitaa CCM asilimia 67.90 na Chadema 25.63 

Leo mkurugenzi wa uchaguzi tawala za mitaa na serikali za mitaa (tamisemi) Khalist Luanda ametangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku chama cha mapinduzi kikipata ushindi katika vjiji 7290 na chadema 1248 kati ya vijiji 9047.

Akitangaza natokeo hayo mkoani Dodoma Luanda alisema katika katika mitaa ccm imepata 2116 na Chadema ikipata 753 Cuf 753 kati ya mitaa 3078.

Aliitaja mikoa ambayo imefanya zoezi hilo bila ya kuwa na vurugu huku akiipongeza kuwa ni dodoma njombe singida katavi pwani mbeya kagera ruvuma arusha mtwara Lindi.

Alisema mikoa ambayo ilikuwa. Na dosari katika zoezi hilo kuwa ni kigoma katika eneo la kasulu tabora. Eneo la kaliua na pwani katika eneo la Mkuranga.

Alisema kwa wale wanaorudia. Uchaguzi hawatakiwa kufanya kampeni kwani wakati wa kampeni uliishapita huku akisema siku ya kufanya uchaguzi ni jumamosi.

"Jumaomosi. Ya wiki hii ndio kwa wale ambao hawajafanya uchaguzi ndio watafanya niwaombe wawe watulivu katika kipindi hichi naamini zoezi letu limeenda vizuri" alisema Luanda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: