Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front,  Dk. Alex Malasusa akitoa baraka kwa waumina wa kanisa hilo  baada ya kumalizika kwa ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Askofu Malasusa akiongoza ibada ya Krismasi leo.
Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay, Padri Stephano Kaombe akitoa mahubiri wakati wa ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi juzi.
Kwaya ya Agape ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Azania Front ikiimba nyimbo za kumtukuza Mungu wakati wa ibada ya Krismasi.
Waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Azania Front.
Kwaya ya Kanisa la Mtakatifu Petro.
Waumini wa Kanisa la Kanisa la Mtakatifu Petro wakiwa katiba ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismasi. (Picha zote na Francis Dande.)
---
Na Mwandishi Wetu

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Dk. Alex Malasusa amesema kuwa tatizo la ufisadi linaloendelea nchini limechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwoga wa viongozi kusita kuwachukulia hatua  watuhumiwa.

Dk. Malasusa amesyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ibada ya Sikukuu ya Krismas ambayo huadhimishwa kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

"Taifa linahitaji viongozi waaminifu na waadilifu kama alivyokuwa Yesu, lakini tofauti ni kwamba lina viongozi wenye asili ya woga na kurushiana, rushiana mpira, sijui nani atakayeweza kulioko taifa letu, hata hii mnayoiita mihimili mingine haitaweza kuliokoa taifa letu," alisema.

Dk Malasusa aliongeza kuwa jambo linaloweza kuliokoa taifa ni kila kiongozi aliyepewa dhamana anatakiwa kuwa mwema na hodari kama alivyokuwa Yesu.

"Viongozi wakiishi kama Yesu katika maisha yao watapata uhodari na ujasiri wa kuchukua maamuzi na ndipo hapo tutapata viongozi wenye huruma, kwa sababu hilo limekosekana katika jamii yetu kuanzia ngazi ya familia, na ndio sababu nimekuwa nisikia watu wakiiba mamilioni lakini sasa imefikia mabilioni kama ni kweli maswali haya yanatakiwa majibu," alisema.

Dk Malasusa, alisema kuwa kutokana na hali mbaya ya ubadhilifu inayolikumba Taifa hili inaonyesha wazi kuwa Yesu anahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote ili aweze kulinusuru taifa hili na sio kutegemea uzuri wa sheria zilizopo kuwa mkombozi wa taifa hili.

"Kama uzuri wa sheria tulizo nazo ungekuwa msaada basi tusingeshuhudia magereza zikijaa na vijana wangeweza kuondokana na mateso waliyo nayo, hayo yote hayataweza kufanikiwa kwa uzuri wa viongozi tulionao na wala si maneno yao mengi wanayotuahidi," alisema.

Dk. Malasusa alisema kuwa sikukuu hiyo itumike kuwabadilisha wanadamu kwa kuishi maisha yanayompendeza Mungu ndiyo itatoa haki ya kusherehekea sikukuu ya Krismas.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: