Mafundi wa Kampuni ya Beijing Construction and Engineering Group (BCEG) wakiendelea na ujenzi wa kuta za vyumba vya jengo la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza.
 3798 na 3820 na 3821
Nguzo utakapojengwa mtambo wa kufua umeme katika kiwanja cha ndege cha Mwanza zikiendelea kujengwa na mkandarasi, BCEG ya China.
Ujenzi wa ghala la mizigo la kiwanja cha ndege cha Mwanza ukiwa katika hatua za awali. Aliyesimama ni Mhandisi Abdallah Dhahiri wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) anayesimamia ujenzi huo.
Jengo la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza kama linavyoonekana likiendelea kujengwa katika moja ya vilima jirani na kiwanja hicho.
Ndege ya Fastjet ikijongea kwenye maegesho ya ndege ya kiwanja cha ndege cha Mwanza baada ya kutua. Urefushaji wa barabara ya kutua na kuruka ndege unaofanywa na BCEG ya China unaendelea vizuri ambao tayari mkandarasi ameanza kuweka tabaka la kokoto.
Jengo la kuongozea ndege katika kiwanja cha ndege cha Mwanza kama linavyoonekana kwa mbali juu kilimani.
Meneja wa kiwanja cha ndege cha Mwanza, Esther Madale.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: