Maelekezo Muhimu.
  1. Wahitimu wa kidato cha sita mwaka 
    2014, kidato cha nne mwaka 2013 na JKT Mafinga, Mlale, Ruvu, Mgambo, 
    Bulombola, Kanembwa, Itende, Nachingwea, Mbweni, Maramba, Chita, 
    Makutupola, Mtabila, Msange, Mgulani, Oljoro, Rwankoma na Kimbiji 
    wamechaguliwa kujiunga na mafunzo ya awali ya Jeshi la Polisi.
  2. Wahitimu hawa waliochaguliwa 
    wanatakiwa kuripoti tarehe 28/11/2014 kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa 
    kama ilivyooneshwa kwenye jedwali hapa chini ili waandaliwe usafiri wa 
    kuwapeleka Shule ya Polisi Tanzania tarehe 30/11/2014.
  3. Zoezi la usajili litaanza 
    shuleni hapo tarehe 01/12/2014 hadi tarehe 15/12/2014. Atakaefika kuanzia 
    tarehe 16/12/2014 hatapokelewa.
  4. Atakaeamua kuripoti kwa Kamanda 
    wa Polisi ambako hakupangiwa atalazimika kujigharimia usafiri hadi Shule 
    ya Polisi Tanzania mjini Moshi.
  5. Vijana hawa watalazimika kufika 
    shuleni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
    1. Vyeti vyao vyote vya masomo (original Academic Certificates/Result slip pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa (Original Birth 
      certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
    2. Mashuka mawili rangi ya Bluu 
      Bahari (light blue)
    3. Chandarua chenye upana futi 
      tatu
    4. Nguo za michezo(Track suit 
      nyeusi,Tshirt blue na Raba)
    5. Pasi ya Mkaa Ndoo moja
    6. Pesa za kulipia bima ya afya 
      kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=).
    7. Pesa kidogo ya kujikimu.
  6. Kwa mujibu wa kanuni za shule 
    ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya mkononi. Atakayepatikana 
    na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na kusaidia kufanya 
    mawasiliano.
  7. Angalia orodha kwenye tovuti ya 
    Ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest barabara ya 
    mahakama kuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: