Moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha likishushwa katika Bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), leo limepokea mabehewa 50 ya kubebea makasha ambapo mradi huu unatekelezwa chini ya Mpango wa Matokeo makubwa sasa(BRN).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akisistiza jambo wakati wa kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha, leo katika Bandari ya Dar es Salaam. Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaomba Menejiment ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kuyatunza lakini pia na wananchi wanaokaa pembezoni mwa reli kusaidia Serikali kutunza miundombinu ya reli.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Aman Kipalo Kisamfu, kabla ya kupokea mabehewa 50 ya kubebea makasha katika bandari ya Dar es Salaam, leo asubuhi. Kulia kwa Mhandisi Kipalo Kisamfu ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Alois Matei.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk . Shaaban Mwinjaka (mwenye tai ya blue), akiangalia behewa moja kati ya mabehewa 50 ya kubebea makasha yalishuhushuwa katika bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuniya reli Tanzania (TRL), Mhandisi Amani Kipalo Kisamfu. Kuwasili kwa mabehewa hayo kutasaidia kupunguza msongamano wa mizigo ya makasha na kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam.

(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikali-Uchukuzi).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: